MCHEZAJI nafasi ya ulinzi wa timu ya Shooting Stars nchini Nigeria, Izu Joseph  amepigw arisasi na kufa akijiandaa kuingia uwanjani mjini Bayelsa.
Mchezaji huyo alikuwa mmoja wa timu ya  Oluyole Warriors ambayo ilimaliza nafasi ya 14 katika msimu uliopita (2015/2016) wa kinyang’anyiro cha Nigerian Professional Football League ambapo Enugu Rangers ndio mabingwa.
Twita kutoka katika klabu hiyo yenye makao makuu yake mjiniIbadan  iliandika; “A Shooting STAR is gone! Izu Joseph is gone! Flamboyant defender is gone! RIP, brother. What a life! May God strengthen his family #Tragedy.”
inasadikiwa kwamba mchezaji huyo alipigwa na risasi iliyotoka katika uwanja wa mapambano kati ya vikosi vya nchi hiyo Joint Task Force (JTF) vinavyokabiliana na wanamgambo katika delta za Niger Delta Oktoba 16 mwaka huu.
 Izu Joseph alijiunga na Shooting Stars mwaka  2014 kutoka timu ya  Bayelsa United wakati timu hiyo ya Ibadan ikiwa nafasi ya Nigeria National League.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO