Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais , Dk John Magfuli  akiwasalimia baadhi ya wazee wasiojiweza na wenye ulemavu wa viungo  wanaoishi katika Kambi ya Wazee  wasiojiweza ya Fungafunga , iliyopo Manispaa ya Morogoro,  wakati alipowatembelea kuwasalimu pamoja na kuwakabidhi misaada ya aina mbalimbali ikiwemo viroba vya unga wa sembe  ulitokana na mchango wa wadau mbalimbali  waliomuunga mkono.


Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais, Dk John Magfuli akimkabidhi msaada wa vitu mbalimbali ukiwemo viroba vya unga wa sembe kwa Mwenyekiti wa Wazee wasiojiweza wa kambi ya Fungafunga , iliyopo Manispaa ya Morogoro, Joseph Paulo Kaniki , jana  ( Okt 13) wakati alipowatembelea kuwasalimu na kuwakabidhi misaada hiyo ambao ilitokana na mchango wa wadau mbalimbali waliomuunga mkono.

 Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais , Dk John Magfuli  akiwasalimia baadhi ya wazee wasiojiweza na wenye ulemavu wa viungo  wanaoishi katika Kambi ya Wazee  wasiojiweza ya Fungafunga , iliyopo Manispaa ya Morogoro,

Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli , akiwa pamoja na baadhi ya watoto wa kijiji cha Chazi, Kata ya Sungaji,Tarafa ya  Turiani, wilayani Mvomero , mkoa wa Morogoro , alipotembelea kambi ya wazee na watu wenye mahitaji maalumu ya Chazi na kukabidhi zawadi ya vyakula kwa wazee hao.

Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli ,akimsabahi kwa kumshika mkono mtoto wa  wa kijiji cha Chazi, Kata ya Sungaji,Tarafa ya  Turiani, wilayani Mvomero , mkoa wa Morogoro , wakati alipotembelea  kambi ya wazee na watu wenye mahitaji maalumu ya Chazi  na kukabidhi  zawadi ya vyakula kwa wazee hao.


Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli , akipokea mkungu wa ndizi kutoka kwa Devotha Ngapata  ambaye ni mfanyakazi wa Kambi ya Wazee na watu wenye mahitaji maalumu ya Chazi, Turiani, wilayani Mvomero , mkoa wa Morogoro, alipomkabidhi kwa niaba ya wenzake kumuunga mkono kusaidia wazee wanaishi kambini hapo.Picha zote na John Nditi wa HabariLeo

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO