TANZIA
Katibu Mkuu ,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto anasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi wake ambaye alikuwa Mkurugenzi Msaidizi,Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma,Bi.Hellen Semu,kilichotokea leo mchana tarehe 16/10/2016 kwa ajali ya gari eneo la Mkwazu kwa Msakamali,Wilayani Chalinze akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma kikazi.
Taarifa zingine za msiba zitatolewa baada ya kuwasiliana na familia ya Marehemu.
Katibu Mkuu anawapa pole Familia ya Marehemu pamoja na wafanyakazi wote wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto.
BWANA ALITOA,BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.AMEN
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(Afya)
16/10/2016


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO