GAZETI moja la Dailysun SA limeandika habari ambayo inaonekana kama kituko kuhusu na mwanaume mmoja kubakwa na wanawake wawili kisha kuibiwa kila kitu chake ikiwamo gari lake la kifahari Mercedes Benz.
Mtu huyo amedai kwamba alipumbazwa kwa mihadarati kabla ya kubakwa na kuibiwa kila kitu.
Imeelezwa kuwa mtu huyo aliwasili nyumbani kwake East Park, maeneo ya Kagiso, Mogale City  nchini Afrika Kusini kutoka katika pilikapilika za wikiend na  akiwa anaegesha gari lake wanawake wawili walimfuata na kusema kwamba wameponea tundu la sindano kubakwa na genge kubwa la wahuni.
Wanawake hao walisema kwamba wanahitaji  ulinzi; na kwa kuona kwamba shida yao aliwaalika ndani wapumzike kidogo kabla ya kuendelea na safari yao.
Alisema wakiwa hapo waliamua kupta kinywaji lakini anachokumbuka ni kuamka saa tatu asubuhi akiwa kama alivyozaliwa na alipojitazama akagundua kwamba amebakwa.
Aidha alipoangalia gari lake halikuwepo.
Vitu vingine ambavyo vilitoweka pete yake ya ndoa, kadi za benki, simu, leseni ya udereva, mfuko wake wa safari na Samsung Galaxy Grand Prime
Msemaji wa polisi wa Kagiso  kapteni Solomon Sibiya  amesema kwamba polisiw anafanyia uchunguzi wizi huo ingawa hawajafungua shauri la kubakwa.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO