Waziri Nape akiwasilisha WADAU wa habari leo wanaanza kuujadili muswada wa sheria ya huduma za

habari huku wabunge wakisema jambo hilo linahitaji mjadala mrefu ili
kulinda maslahi mapana ya tasnia ya habari na wanahabari nchini.

Wakizungumza jana mara baada ya Waziri wa   Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Nape Nnauye kuwasilisha hati ya muswada huo mbele ya
kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii baadhi ya
wabunge walitaka waandishi wa habari kama wadau muhimu washiriki kutoa
maoni yao kwenye kamati hiyo ya bunge.
Mbunge wa Buyungu ,Kasuku Billago (Chadema), alisema muswada huo
umekuja kwa wakati muafaka na  kuwataka waandishi wa habari kukomaa
katika suala linalohusu.
“Haki nyingi za waandishi wa habari hazijaelezwa kwenye muswada huo,
suala lingine la kuhoji ni nani mwenye mamlaka ya kufuta chombo cha
habari kwani kosa moja linafanya chombo kizima kifungiwe” alisema
 Alisema chombo ni taasisi kinatoa ajira na adhabu iwe inalenga kwa
aliyetenda kosa.
“ Chombo ni taasisi inayotoa ajira aadhibiwe mtu sio taasisi ili
kuwezesha taasisi husika kuendelea kuwepo kuna watu maisha yao
yanakuwa mle mnapofungua hata familia zinaathirika” alisema
inahitaji linatakiwa kufanyika kwa umakini mkubwa kwani serikali
imekuja na lengo jema lakini kuna vitu ambavyo vinatakiwa kujadiliwa
kwa kina ili kuwe na tija kwa kila upande wenye maslahi.
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia alisema unahitajika mjadala mrefu sio
jambo la kukurupuka.
“Serikali imekuja na lengo jema ila kuna vitu ambavyo vinatakiwa
kujadiliwa kwa kina “ alisema
Alisema kwa mtazamo wake kama muda hautoshi haiwezi kuzuia wadua kutoa maoni.
“Sio lazima kitu kiletwe leo na kupita, unaweza kufutwa pia ukatetwa
tena kwa majadiliano ya kina” alisema
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe aliwataka waandishi wa habari
kama wadau muhimu kushiriki kutoa maoni yao.
“Kama mwandishi wa habari ukikatazwa kuingia kwenye kamati kusikiliza
majadiliano ingia kama mdau ili uweze kutoa maoni yako, maoni yenu ni
muhimu sana katika muswada huu” alisema
Hoja hizo za wabunge zimekuja baada ya Waziri Nape kuwasilisha hati ya
muswada huyo kwa kamati ya bunge  ya huduma na maendeleo ya jamii,
alisema lengo la muswada huo ni kuweka masharti ya kukuza na
kuimarisha taaluma na weledi katika tasnia ya habari nchini pamoja na
kuundwa kwa bodi ya ithibati ya wanahabari,Baraza huru la habari
pamoja na kuweka mfumo wa usimamizi wa huduma za habari.
Nape alisema Muswada wa sheria ya huduma za habari umeandaliwa ili
kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika tasnia ya habari
nchini ambazo ni pamoja na upungufu wa sheria zinazosimamia tasnia ya
habari na mabadiliko ya teknolojia ya habari.
Pia alisema changamoto ya kutokuwepo kwa udhibiti wa mzuri na
usimamizi madhubuti ya viwango kwenye taaluma ya habari na utangazaji
kumechangia madhila kwa jamii ikiwemo kuandikwa habari za
upotoshaji,zinazokiuka maadili na zinazoweza kusababisha
chuki,machafuko na uvunjifu wa amani.
‘’Hivyo kuifanya serikali na wadau wengi wengine kuona umuhimu wa kuwa
na sheria kama hii itakayoainisha bayana sifa na viwango vya kitaaluma
katika tasnia ya habari.kukamilika kwa sheria hii kutapanua wigo kwa
wananchi kupata haki yao ya kikatiba yak upata habari’’alisema
Nape alisema kutokana za muingiliano wa teknolojia mwaka 2003 serikali
iliona kuna umuhimu wa kuunganisha vyombo hivi viwili Tume ya
Mawasiliano na tume ya Utangazaji ili kuleta ufanisi  wa usimamizi wa
sekta na utoaji wa huduma bora kwa walaji.
‘’Kwa ujumla sekta hii changamoto kubwa ni taaluma ya habari
kutotambulika kama taaluma kamili inayopaswa kuheshimiwa,kukosekana
vyombo madhubuti na huru vya usimamizi  na badala yake mambo mengi
kuwa chini ya serikali moja kwa moja’’alisema
Pia alisema changamoto nyingine ni wadau wa habari kutoshirikishwa
kikamilifu katika utungwaji wa sheria zilizopo hivyo kutokidhi matakwa
ya wadau katika sekta ya habari.
‘’Sheria hii inaleta mageuzi makubwa katika usimamizi wa sekta ya
habari hapa nchini ni sheria mabyo inakwenda kwa mara ya kwanza katika
historia ya nchi yetu,kuifanya rasmi sekta ya habari kuwa sekta
rasmi’’
Aidha alisema ushahidi uliowazi kwamba waliowengi wamekuwa waathirika
wa kadhia ya uandishi usiozingatia maadili na weledi wa taaluma ya
habari na utangazaji kwa kukashifiwa au kuzushiwa taarifa zisizokuwa
na ukweli wowote.
Alisema mapendekezo yaliyomo katika sheria ya habari kwa kiasi kikubwa
yamelenga kutatua changamoto ya kuwa na wanahabari waliosomea kazi yao
na ambao waewekeana wao wenyewe maadili ya kufuata.
Pia alisema changamoto ya kukuwa kwa teknolojia ya habari na
utangazaji kumefanya sheria zilizokuwa zikisimamia  tasnia ya habari
na utangazaji kupitwa na wakati na kutoendana na
‘’Ni sheria itakayoleta mifumo ya kisasa ya usimamizi na ni mifumo
ambayo inaweza kugusa au kubadili namna tutakavyotenda na
tunavyofikiria sasa,niwaombe wanatasnia wenzangu tuwe tayari kwa
mabadiliko ili taaluma yetu iheshimiwe na sisi  wenyewe tuheshimike
zaidi’’alisema
Nape alisema serikali imeona kwa sasa ni muhimu kuwa na sheria ambayo
itakidhi pia matakwa ya Matumizi ya Teknolojia katika sekta ya habari.
‘’Hivi sasa magazeti ambayo yalikuwa yakitolewa kwa njia ya nakala
ngumu kwa sasa yanaweza kutolewa njia ya mtandao wa internet na
wananchi wanawe kuyasoma katika mfumo huo’’alisema
Nape alisema mambo muhimu na matokeo ya sheria inayopendekezwa
kutungwa ni kama kuwepo kwa sheria inayoendana na sera ya habari na
utangazaji, kuwepo kwa mfumo madhubuti ya kisheria wenye kukidhi
mahitaji katika eneo la usimamizi na uendeshaji wa taaluma ya uandishi
wa habari na utangazaji.
Alisema sheria hiyo inaleta mageuzi makubwa katika usimamizi wa sekta
ya habari hapa nchini.
Ni sheria ambayo inakwenda kwa mara ya nkwanza katika historia ya nchi
yetu, kuifanya sekta ya habari kuwa taaluma kamili
Source: Sifa Lubasi

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO