WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kupatiwa orodha ya wadaiwa sugu
wa taasisi zote za serikali Mkoani Dodoma ambao malimbikizo yao ya
ankra za maji yamefikia sh. Bilioni 1.4.
Alisema hayo jana katika siku ya pili ya ziara yake mjini hapa  baada
ya kutembelea chanzo cha maji cha Mzakwe
Aliagiza kupatiwa kwa orodha ya wadaiwa sugu wa taasisi zote za
serikali Mkoani Dodoma ambao malimbikizo yao ya ankara za maji
yamefikia Sh. Bilioni 1.4.
Alisema mtu au taasisi inayopata huduma ya maji, kuhakikisha wanalipa
bili kwa muda muafaka ili kuepukana na kulimbikiza madeni makubwa.
“Niletee haraka orodha ya wadaiwa wote wa Ofisi za serikali na taasisi
za umma ambao hawajalipa bili zao. Madeni yote ni lazima
yalipwe,”alisema Majaliwa
Aidha Waziri Mkuu alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme
kuwaondoa wavamizi wote ambao wamekuwa wakiendesha kilimo na uchomaji
mkaa
Alitaka eneo hilo lilindwe  kwa nguvu zote kutokana na serikali
kutumia gharama kubwa kutengeneza miundombinu inayoharibiwa kwenye
vyanzo vya maji.
Alimtaka mkuu wa wilaya hiyo, kuhakikisha anatumia njia yoyote
kuwaondoa wavamizi hao ambao wanasababisha upungufu wa maji hali
inayowafanya wengine kukosa maji.
Pia aliitaka Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa mazingira mjini  Dodoma
(Duwasa), kuhakikisha wanasambaza maji maeneo ambayo Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Makuu (CDA), wanatarajiwa kupima viwanja.
Alisema Mji utakuwa na wageni wengi, hivyo Duwasa wanatakiwa
kuhakikisha wanapeleka huduma hiyo na wananchi watakapopata viwanja
wakute tayari maji yamefika sambamba na umeme kutoka Tanesco.
Pia Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Duwasa kuhakikisha taasisi za
serikali zinazodaiwa madeni makubwa ya bili za maji, zisionewe aibu na
kutakiwa kuzidai na kulipa.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Duwasa, Mhandisi David Pallangyo,alisema
Mamlaka hiyo ina visima 24 vya kuzalishia maji vikiwamo 10
vinavyozalisha kwa mfumo wa kieletroniki.
Alisema pia kuna visima vingine vya akiba vya kuzalisha maji, wakati
upande wa mashariki vikiwapo visima 10 na magharibi 10 vikiwa na mita
za ujazo kati ya 630 na 800.
Hata hivyo, Pallangyo alisema mamlaka yake bado ina changamoto ya
kuweza kuwafikia baadhi ya wateja, mabwawa ya maji taka na madeni
makubwa ya wateja wao hususani taasisi za serikali.
Pia akizungumza katika kituo cha kusambaza umeme cha Zuzu Waziri mkuu
alilitaka Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kuendelea na kazi ya
kuongeza nguz na kufungua njia mpya ili kuongeza usambazaji.
Alisema Dodoma hakuna shida ya Umeme viwanda vikubwa na vidogo
havitapata shida ya umeme.
Awali meneja ya Tanesco Mkoa wa Dodoma , Zakayo Temu alisema
wamejipanga kuimarisha huduma za upatikanaji wa umeme kwani umeme uko
wa kutosha na wanaohamia Dodoma wasiwe na hofu.
SOURCE: Sifa Lubasi,

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO