Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fisoo (kushoto) akifafanua jambo  wakati wa majadiliano na wanatasnia wa filamu Mkoani Morogoro

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye  ameeleza kuwa ili kuwa na filamu bora ni budi wanatasnia wa  filamu kuzingatia taaluma na weledi katika kazi zao.
Dkt. Makoye aliyasema hayo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanatasnia wa filamu yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu kwa lengo kuboresha filamu za ndani Mkoani Morogoro ambapo aliwasilisha mada kuhusu umuhimu wa weledi na taaluma katika filamu.  
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye akiwasilisha mada  kuhusu umuhimu wa weledi na taaluma

Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Mona Mwakalinga akiwasilisha mada kuhusu uaandaji wa filamu ikiwemo uandishi wa miswada ya filamu,utafiti na uongozaji 

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo(Kulia) kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akisisitiza umuhi mu wa filamu katika kukuza lugha ya Kiswahili

Bw. Haviti Makofi akiuliza swali wakati wa mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania kuwajengea uwezo wanatasnia hao Mkoani Morogoro

Mmoja wa mwantasnia ya filamu Bibi. Mwajabu Munna akiuliza swali wakati wa mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania ya kuwajengea uwezo wanatasnia hao Mkoani Morogoro.

Baadhi ya  wanatasnia wa filamu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wawezeshaji katika mafunzo   maalum ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wasanii hao katika utayarishaji wa kazi zao Mkoani Morogoro.

Baadhi ya  wanatasnia wa filamu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wawezeshaji katika mafunzo   maalum ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wasanii hao katika utayarishaji wa kazi zao Mkoani Morogoro.

Aliongeza kwa kusema kukosekana kwa  uzingatiaji wa taaluma na weledi, kumefanya baadhi ya kazi kufanywa kwa kulipuliwa,kutojali ubora,kushindwa kubuni na kujikuta wakiishia kunakiri kazi za nje huku kazi zao nyingi zikiwa hazizingatii mambo muhimu kwa kisingizio cha bajeti kuwa kubwa.
“Ni muhimu kwa watayarishaji wa filamu kuwa na taaluma na weledi wa kutosha katika tasnia hii sambamba na kujifunza kupitia warsha,semina na mafunzo mbalimbali zinazoandaliwa na wadau wa filamu ili waweze kutengeneza filamu bora  ”alisema Dkt.Makoye.
 Naye Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Mona Mwakalinga alitoa wito kwa watayarishaji wa filamu kuzingatia mambo makuu matatu wakati wa uaandaji wa filamu ikiwemo uandishi wa miswada ya filamu,utafiti na uongozaji .
“Filamu nzuri huanza na uandishi wa miswada na kufanya utafiti kwa kina ili kutoa muongozo mzuri wa filamu na hatimaye kuzalisha filamu bora “alisema Dkt.Mona.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fisoo aliwataka wanatasnia wa filamu kuzingatia yale yote waliojifunza kupitia wawezeshaji wa mada mbalimbali zilizotolewa katika mafunzo hayo ili kukuza tasnia ya filamu.
Source: Na Lorietha Laurence-Morogoro


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO