Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge akiongea na wenyeviti wa kijiji.watendaji wa kata ,vijiji na maafisa Tarafa wa wilaya ya Tunduru wakati wa kikao cha kutoa maaelekezo ya usimamizi wa msimu wa ununuzi korosho kwa mfumo wa stakabadhi ghalani 2016/2017 Leo mjini Tunduru.

Wakulima wa korosho wa korosho wilaya ya Tunduru wamehakikishiwa uahakika wa fedha o za mauzo ya korosho msimu huu ambapo mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani utatumika.
Kauli hii imetolewa jana mjini Tunduru na Mkuu  Mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge alipokuwa akifungua kikao cha watumishi wa serikali ngazi ya Tarafa,kata na kijiji unaolenga kuwajengea uewzo wa kusimamia ununuzi wa korosho
Mkuu wa Mkoa amewaagiza wenyeviti wa kijiji,watendaji wa kata,vijiji na maafisa Tarafa kuhakikisha wakulima wanauza korosho zao kwenye maghala yaliyoanishwa vijijini ili kusubiri mnada wa korosho zao.
Mfumo wa stakabadhi ghalani umelenga kumsaidia mkulima kupata bei nzuri ya korosho zao kwa njia ya minada itakayozunguka kwenye maeneo yao hivyo wakulima watakuwa na uhakika korosho zao.
Amesema vyama vya msingi vya ushirika vitasimamia ukusanyaji wa korosho ya wakulima kwenye maghala yaliyoanishwa na kutoa risiti kwa mkulima ili kusubiri mnada
 
Sehemu ya wenyeviti wa kijiji.watendaji wa kata,kijiji ,maafisa Tarafa na maafisa ugani wa kata wakiwa kwenye kikao cha kuwajengea uwezo wa kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani utakotumika kununua korosho ya wakulima wa wilaya ya Tunduru msimu huu 2016/2017
Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Dkt.Mahenge amewataka watendaji hawa wa serikali kuhakikisha wanadhibiti biashara haramu ya korosho maarufu Kangomba inayowanyonya wakulima kwa kuwapa bei ndogo ya korosho
“Serikali inategemeakuona mnasimamia kikamilifu msimu wa ununuzi wa korosho na kudhibiti watu wanojihushisha na biashara ya kangomba kwenye kijiji vyenu kwani mnawatambua” Dkt.Mahenge
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera amesema ni aibu kwa wilaya yake ya Tunduru kushindwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani kwani Mkoa mingine inatumia mfumo na kupata bei nzuri.
Mara ya mwisho Tunduru ilitumia mfumo wa stakabadhi ghalani msimu wa 2009/2010 ambapo ilikumbana a changamoto ya wakulima na wadau kutokuuelewa na kushawishi usitumike
Akitoa mada kuhusu umuhimu wa mfumo stakabadhi ghalani msimu mkurugenzi wa masoko wa Bodi ya Korosho Tanzania Juma Yusuf amesema mfumo huu unayo manufaa makubwa kwa wakulima ya kuwapatia bei nzuri ambapo msimu uliopita bei ilifikia kiasi cha shilingi 2800 kwa kilo tofauti na Tunduru walionunua kwa bei ya shilingi 1200
Hivyo amewataka wakulima na uhakika kuwa korosho yao itauzwa kwa bei nzuri na kuwapa thamani nzuri ya korosho zao.
Kuhusu takwimu za uzalishaji amesema Tunduru msimu a 2014/2015 ulizalisha tani 200,000 za korosho na matarajio ya msimu huu ni kuzalisha tani 250,000.
Msimu wa ununuzi korosho ulifunguliwa mwanzoni kwa mwezi wa nane mwaka huu hivyo kulazimu kuwa na vikao vya uhamasishaji wakulima na wadau kuuelewa mfumo wa stakabadhi ghalani.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO