Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari kusiana na huduma mpya ya linda simu ya Airtel Simu Bima itakayowasaidia wateja wote wanaotumia Simu za Smartphone kuziwekea Bima simu zao na kulipia kupitia huduma ya Airtel Money, kulia ni Meneja wa Airtel Money Bw, Moses Alphonce na kushoto ni Muwakilishi wa shirika la Bima la UAP bw, Charles Matondane

WATEJA wa simu wanaotumia simu za kisasa za smartphone wamezinduliwa huduma ya  kuziwekea bima simu zao pindi zinapopotea au kuibiwa.
Huduma hiyo imewezeshwa na Kampuni ya simu za mkononi Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya UAP .
Huduma hiyo imezunduliwa jana na kwamba bima hizo zitalipwa kupitia huduma ya Airtel Money.
Huduma hiyo mpya  ya “Airtel SimuBima” itawawezesha wateja wa Airtel pamoja na watumiaji wote wa Smartphone nchini kuepuka hasara pale simu inapopotea au kuibiwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema kampuni yake imeongeza sababu nyingine kwa wateja wao kuendelea kufurahia huduma zao.
“Mteja ambaye ameibiwa simu yake au kuipoteza basi kupitia huduma hii ya ‘Airtel SimuBima’ tutampatia pesa ili aweze kununua simu nyingine atakayotaka na kisha simu iliyopotea itazimwa moja kwa moja isiweze kutumika tena” alisema Mmbando.
Akifafanua zaidi alisema:“Mteja wa Airtel ataweza kufaidi huduma ya “Airtel SimuBima” mara baada ya kupakuwa aplikesheni ya simuBima kutoka kwenye Playstore na kusajili taarifa za smartphone yake ikiwemo IMEI namba pamoja na gharama ya simu yake  na papohapo atapata ujumbe utakaomwambia gharama ya Bima ya simu hiyo kwa mwaka ambayo ataamua kuilipa yote au kuwa anailipa kwa kila mwezi.”
Alisema kwa mpango huo wa ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na shirika la bima la UAP kupitia ‘Airtel SimuBima’  unahamasisha watumiaji wa simu za mkononi kununua simu orijino ili waweze kufurahia huduma hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa UAP Bw, Raymond Komanga alisema “tunawahakikishia wateja wote wa Airtel watakaosajili namba zao katika huduma ya Airtel SimuBima kwamba tutawalipa madai yao haraka sana pale wanapopatwa na tatizo la kupoteza simu au kuibiwa simu zilizowekewa Bima ndani ya siku tano tu tokea pale wanapotoa taarifa kituo cha polisi na kutujulisha sisi.”

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO