Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge(aliyechuchumaa) akishiriki kazi ya kupanga tanuru la tofali tayari kwa kuchoma na wananchi wa kijiji cha Ligoma Tarafa ya Namasakata wilaya ya Tunduru

Wilaya ya Tunduru umezindua kampeni ya uchomaji tofali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa matundu ya vyoo kwenye shule za msingi na sekondari
Uzinduzi huo umefanywa jana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge alipofanya ziara ya kikazi kijiji cha Ligoma Tarafa ya Namasakata
Katika kuunga mkono juhudi za wananchi mkuu wa Mkoa ameshiriki kazi ya kupanga tanuri la matofali yaliyofyatuliwa na wananchi ili kuwezesha kijiji kujenga matundu ya vyoo kwenye shule ya msingi Ligoma
Katika uzinduzi huu jumla ya matofali 200,000 yamefyatuliwa na wanakijiji cha Ligoma mwezi uliopita ambapo kazi ya uchomaji itatumia Siku kumi na ñne hadi kukamilika.
Akitoa taarifa ya utekelezaji a kampeni ya benki tofali kwenye wilaya ya Tunduru mkuu wa wilaya hiyo Juma Homera alisema jumla ya tofali 7,070,000 zimefyatuliwa kwenye Tarafa zote saba za Tunduru
Aliongeza kusema wilaya yake imejipanga kukamilisha zoezi la matofali na kuahidi kuwa ifikiapo mwezi Desemba mwaka huu watakamilisha ujenzi wa vyoo kwani halmashauri kupitia makusanyo ya ndani watatoa vifaa vya kiwandani 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge akikagua kazi ya kupanga tanuru la tofali aliposhiriki uzinduzi wa uchomaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule ya msingi Ligoma wilaya ya Tunduru Jana

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akiwa na mbunge wa Tunduru Kusini IDD Mpakate wa pili  kushoto wakishiriki kazi ya kupanga tanuru la tofali pamoja na wananchi wa kijiji cha Ligoma wilaya ya Tunduru Jana.

Wakati huo huo mkuu wa Mkoa alikagua hali ya matundu ya vyoo kwenye hule ya msingi Ligoma na kujionea upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo vya wanafunzi
Shule ya msingi Ligoma yenye wanafunzi 656 na na walimu 8 ina matundu ya vyoo sita na upungufu uliopo ni matundu ya vyoo 24 wakati mahitaji kwa wasichana ni 18 na wavulana ni 12.
Dkt.Mahenge amewapongeza wilaya ya Tunduru kwa jitihada walizofikia kupata matofali na kuwataka waanze kuchimba matundu ya vyoo
Choo kilichomsikitisha mkuu was Mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith Mahenge cha  wanafunzi wa shule msingi Sasawala wilaya ya Namtumbo. Choo kilichojengwa  kwa nyasi kinatumiwa na zaidi ya wanafunzi 400 wanatumia. Mkuu huyo sasa anafanya ziara za kuhimiza ufyatuaji wa matofali kwa ujenzi wa vyoio bora na imara katika shule za mkoa

“Nawataka sasa muanze hatua ya pili kwa kuchimba mashimo ya vyoo ili halmashauri ya wilaya ilete saruji,nondo,mabati,na masinki na kuweka mfumo wa maji” alisisita mkuu wa mkoa
Mkuu wa Mkoa amewataka na kuwasisitiza wakuu wa wilaya zote kutembelea na kukagua hali ya miundombinu ya vyoo,madarasa na nyumba  za walimu ili matofali yanayofyatuliwa sasa na wananchi yatumike kukamilisha ujenzi ya mundombinu hii muhimu.
Aidha amewaagiza maafisa Elimu wote wa wilaya kutokaa ofisini na kutayarisha takwimu na zisizo na uhalisia.
Dkt.Mahenge alizindua kampeni ya ufyatuaji tofali kwenye Mkoa wa Ruvuma mwezi Agosti mwaka huu na kuelekeza kijiji vyote kuwa na benki tofali 100,000 zitatumika kujenga matundu ya vyoo kwenye shule,zahanati kwenye kijiji visivyo na zahanati.
Alisema ni lengo la Mkoa kuona unanza mwaka  2017 ukiwa umekamilisha ujenzi namatundu ya vyoo kwenye shule za msingi na sekondari ili kuwawezesha wanafunzi kusoma kwenye mazingira ya usafi.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO