Peter Laizer,  akiwaeleza umeme wa zola unavyofanyakazi
KAMPUNI ya kuuza umeme wa nishati ya jua, Zola ya Jijini dare s salaam imepanua wigo wake na sasa bidhaa zake zinapatikana Tanga.

Akizungumza kwenye ufunguzi huo,Meneja mauzo kanda ya Kaskazini Tanga na Kilimanjaro, Peter Laizer, amewataka wajasiriamali wadogowadogo  kutumia umeme wa Zola kwa  kuwa ni wa gharama nafuu.

Amesema wajasiriamali wa mbogamboga na matunda wanaweza kuinua kipato chao kwa kusindika bidhaa zao wakitumia mashine zinazoendeshwa na nishati ya jua ya Zola ili waweze kuzihifadhi na kusafirisha kwenda katika masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
                                           
Amesema umeme huo ni mkombozi kwa watu wa kipato chote, cha chini, kati na juu na, umeme huo utaondolea adha mbalimbali kama za kuchaji simu mbali na nyumbani na ufuatiliaji wa taarifa katika Luninga pamoja na kusaidia watoto kusoma katika mwanga bora  nyakati za  usiku.

 “Umeme huu ni mkombozi kwa wananchi wa Tanga kwani ni rahisi, hauchukui muda kuupata na pia utawasaidia wananchi kuhifadhi kiasi cha pesa ambacho walikuwa wanakitumia kwa nishati nyingine kupata mwanga, Pia humsaidia mwananchi wa kipato cha chini kubadilisha maisha kwa kupata habari, taarifa pamoja na burudani, kwani mbali na taa na kuchaji simu pia utapata Radio na TV za sola”alisema Laizer.
 
wateja wakipata nafasi ya kuangalia redio za Zola zinazotumia nishati ya jua

Amesema umeme huo  umekuwa mkombozi kwa wanafunzi wa vijijini ambao walikuwa hawana uwezo wa kujisomea usiku au husoma katika mwanga hafifu wa vibatari sasa wanapata mwanga  salama kwa afya ya mwili na macho.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Central Tanga, Diana Mussa, amewataka wakazi wa eneo hilo kutumia nafasi hiyo pia kuwezesha usafi wa maeneo yao.
Alisema hayo akizungumza mara baada ya ufunguzi wa duka la kuuza umeme la  Zola lililopo barabara ya Markert Street Tanga juzi.
    source;Tangakumekucha                                            

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO