KIWANDA Cha Saruji Cha Simba Cement kimekabidhi madarasa mawili, matundu mawili ya choo na madawati 50 shule ya  Msingi ya Kange  iliyopo mkoani Tanga.

Msaawote huo una gharama ya zaidi ya shilingi milioni 76.

Msaada huo utasaidia kupunguza kero ya wanafunzi kurundikana katika darasa moja na wengine kukaa chini jambo ambalo hupunguza weledi kwa wanafunzi.
 
 Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias  Mwailapwa akifungua moja milango ya vyumba viwili ya madarasa shule ya msingi Kange Tanga, anayemtazama ni Ofisa Fedha Pitter De Jagger na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Tanga, Daudi Mayeji.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa, alisema msaada huo uwe mfano kwa makampuni mengine na wadau wa elimu ili lengo la kuondokana na changamoto katika  baadhi ya shule lifanikiwe.

Kwa upande wake, Mkuu wa Rasilimali watu kiwanda cha Saruji cha Simba, Anna Malambugi, alisema kiwanda hicho moja ya sera zake ni kusaidia  jamii ikiwemo, Elimu, Afya na Mazingira.
 


Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Noor Mtanga, akiwakabidhi madawati 50 wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange .Nyuma kulia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kasera, Aidan Munis na kulia ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, Debora Mzava


Mkuu Rasiliwamali watu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Anna Mwalambuji akiwakabidhi madawati 50 

Nae Mwalimu mkuu wa Shule hiyo, Debora Danniel, alisema awali walikuwa wakiwaweka wanafunzi 120 darasa moja kufuatia uhaba wa madarasa.


Alisema kwa msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi kurundikana darasa moja na kuwaomba wadau wa elimu kuisaidia shule hiyo katika Nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu yamaji na uchakavu wa majengo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO