taswira ya msanii namna ambavyo wanaotaka kuhifadhiwa watakavyohifadhiwa
MAHAKAMA ya mjini London imetoa ruksa kwa mwili wa binti wa miaka 14 aliyefariki kwa ugonjwa wa kansa kuhifadhiwa katika vimiminika maalumu  kama alivyotaka ili kuja kuamshwa baadae dawa za kansa anayougua itakapopatikana.
Binti huyo ambaye jina lake limehifadhiwa aliomba mahakama kumpa haki ya kuhifadhiwa kwa kuwa hataki kufa akiwa mtoto ingawa anajua ugonjwa anaougua utamuua.
Ruksa hiyo ya kutekelezwa kwa matakwa yake imetolewa huku baba yake mzazi akiwa anapinga mtoto wake kuhifadhiwa kwa kauli kwamba hata kama ataamshwa miaka 100 ijayo au 200 atakuwa hana mtu anayemtambua ambaye ni ndugu yake.
Binti huyo ambaye aliomba nafasi ya kuhifadhiwa katika mfumo huo maalumu akisubiri kuamshwa baada ya dawa kupatikana, ombi lake lilikuwa linaungwa mkono na mama yake mzazi
Jaji wa mahakama kuu  alisema kwamba ombvi la binti huyo ni vyema kusikilizwa na kwamba mama mzazi aruhusiwe kuona namna bora ya kumhifadhi binti yake.
Binti huyo ambaye alikufa Oktoba  mwaka huu mwili wake tayari umeshapelekwa Marekani kwa kuhifadhiwa.
Taarifa ya shauri hilo la aina yake, ndio kwanza imetolewa na mahakama.
Binti huyo ambaye hakutajwa jina lake na ambaye alikuwa anaishi mjini London, Uingereza katika siku za mwisho za uhai alikuwa anajifunza kwa bidii masuala yanayohusu  hifadhi kusubiri kuamshwa baada ya dawa  za ugonjwa kupatikana.
Mfumo huo ambao kiingereza unajulikana kama Cryonics ( neno lililotolewa kutoka Lugha ya kigiriki)  huwezesha kuhifadhiwa kwa mwili wa marehemu katika kiwango cha chini cha joto na mara nyingi ni chini ya hasi 130 sentigredi, kusubiri maendeleo ya sayansi katika ugunduzi wa dawa kwamba mwili huo utatibiwa na kuamshwa kuendelea na maisha.
Imeelezwa kuwa binti huyo alimwandikia Jaji  akimtafadhalisha kwamba anataka kuishi maisha marefu na kwamba hakutaka kuzikwa ardhini bali kuhifadghiwa akisubiri kupatikana kwa dawa ya ugonjwa wake.
Alisema: " kuhifadhiwa kwa namna ninavyotaka kutanipatia nafasi ya kuponywa ugonjwa wangu na kuamshwa hata kama ni miaka 100 ijayo."
Jaji Peter Jackson, alimtembelea binti huyo katika hospitali aliyokuwa akitibiwa na  kufurahishwa na uthubutu wake   na namna anavyoangalia hali yake na ugonjwa ulivyo.
Katika hukumu yake alisema uamuzi huo hauzingatii ubaya au uzuri wa hifadhi bali migongano ya wazazi wawili kuhusu namna ya kuhifadhi mwili wa mtoto wao.
Pamoja na kuwepo na nadharia kuhusu Cryonics  bado  haijajulikana kwa yakini kwamba ni kweli mtu anaweza kumashwa baada ya kufa kutokana na ugonjwa Fulani ambao hauna dawa kwa sasa.
Vituo vya hifadhi kwa mtindo huo viko Urusi na Marekani pekee ambapo mwili unaweza kuhifadhiwa ndani ya kimiminika cha nitrogen katika kiwango cha chini cha joto ( chini ya -130C) .
Gharama za kuhifadhi mwili huo kwa miaka mingi zinakadiriwa kuwa paundi za kiingereza,37,000.
Wazazi wa binti huyo walitengana na kwamba hajamuona baba yake kw amiaka sita kabla ya kuanza kuumwa.
Wakati mama wa binti alikubaliana na ombi la mtoto wake baba mtu alisema si sawa kw ahoja kwamba hata kama dawa itapitakna baada ya miaka 200 hataweza kumpata ndugu yake na kwa kuwa anaingia katika hifadhi akiwa na miaka 14 anaweza kuwa katika msongo mkubwa wa mawazo tena akiwa nchini Marekani.
Ingawa baba huyo alikuja kukubaliana na ombi la mtoto wake katika siku za mwisho za uhai wake,ombi na hukumu hiyo imetoa changamoto kubwa kwa wanasheria kuhusu maendeleo na mwenendo wa sayansi na namna ya kukabiliana na hoja za msingi za kitamaduni na mapokeo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO