TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Novemba, 2016 amemtembelea na kumjulia hali Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martin Shigella ambaye amelazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Bw. Martin Shigella alifikishw ahospitalini hapo tangu Jumatano iliyopita kwa ajili ya kupata matibabu.
Akimpa pole wodini humo Rais  Magufuli amesema“Nakupa pole sana Ndg. Martin Shigella kwa maradhi yaliyokupata, nakuombea kwa Mwenyezi Mungu upone haraka na urejee katika kituo chako cha kazi ili uendelee na majukumu ya ujenzi wa Taifa”
Hali ya Bw. Martin Shigella inaendelea vizuri.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Novemba, 2016

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO