RAIS wa Zambia, Edgar Lungu  amepunguza mshahara wake hadi kufikia nusu ya anayotakiwa kupata kwa lengo la kuonesha mfano katika juhudi za serikali ya nchi hiyo kukabiliana na nakisi ya bajeti.

Kauli ya upunguzaji wa mshahara huo imetolewa na Makamu wa Rais, Inonge Wina.

Mshahara wa Rais wa Zambia ni ZMW mil. 36,000.00

Uamuzi wake huo unakuwa wa pili katika kipindi kifupi. Uamuzi wa kwanza ulihusisha kukataa kwake kutumiwa kwa fedha za Urais kumjengea nyumba na kusema kwamba akimaliza muhula wake atarejea nyumbani kwake Chawama na kukaa kwenye nyumba yake.

Akihutubia Bunge Septemba 18, 2015, Rais Edgar Lungu alisema wazi hataki serikali kumjengea nyumba  akiondoka madarakani.

Alisema utamaduni huo ni mbaya haufai na unaiongezea gharama serikali.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO