TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinalaani vikali vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ambao umekuwa ukifanyika nchini hasa ubakaji na ulawiti wa makusudi ambao wakati mwingine watu hubakwa na kuawa.


Matukio ya ubakaji, ulawiti na mauaji kwa wanawake na watoto yamekuwa yakifanyika kwa kasi ambapo  hivi karibuni lilitokea kwa msanii wa ngoma za asili na Bongofleva ambaye alikutwa amefariki dunia katika majaluba ya mpunga mita chache kutoka barabara ya Moshi-Arusha
Mkurugenzi Mtendaji Edda SangaKwa mujibu wa taarifa za upelelezi wa awali wa kipolisi zimeonyesha kuwa yalitokana na kupigwa, kubakwa na kunyongwa kisha kutupwa eneo la Makumira, Kata ya Usa River wilayani Arumeru, tukio ambalo TAMWA imelilaani vikali na kuomba jeshi la polisi kufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha waliohusika wanatiwa mbaroni na kuchukuliwaa hatua kali za kisheria.


Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania la tarehe 26 Oktoba, mwaka huu lilimkariri Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa kuwa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, katika Manispaa ya Moshi pekee, matukio ya ubakaji yaliyoripotiwa ni zaidi ya 102 ambapo kati ya hayo 33 yalikuwa ni ya ulawiti.


Aidha tukio hilo la kinyama kwa msichana huyo ni miongoni mwa matukio mengi ya kikatili kwa wanawake na watoto hali ambayo inahatarisha na kutishia ustawi wa mwanamke huku baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kuwa vitendo vya ubakaji na ulawaiti  vimeongezeka kwa kasi.


TAMWA inaamini kuwa sheria itafuata mkondo wake ili liwe fundisho kwa wanaoendelea kufanya ukatili wa kinyama kwa wanawake na watoto.

Mkurugenzi Mtendaji
Edda Sanga


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO