![]() |
baada ya pambano kumalizika |
kwa mujibu wa Hindustan on Line iliyokuwa inalipeleka pambano hilo mubashara,Vijender Singh kwa ushindi huo amefanikiwao kutetea taji lake la WBO Asia Pacific Super-Middleweight.
Vijender Singh ambaye kwa mara ya kwanza alikuwa anakabiliana na mpiganaji mwenye rekodi nzuri na aliyepigana mapambano mengi alimmudu Cheka ambaye ni bingwa wa zamani wa dunia.
Kwa mujibu wa Hindustan, Vijender Singh alimdhibiti Cheka toka kuanza kwa pambano hilo baada ya kufanikiwa kumzuia kuingia maeneo yake ya kujihami .
Baada ya kufanikiwa kumdhibiti Cheka, Vijender akaenda mbele 3-1 kabla ya kusukuma ngumi saba dhidi ya tatu za Cheka katika raundi ya pili .
Kwenye raundi ya tatu mpiganaji huyo kutoka Haryana alitawala kilinge kiasi cha marefarii kuamua kumpa ushindi wa technical knockout.
Watanzania waliokuwapo pale wakiendesha heka heka wanasema ni mchezo na mmoja alisema pamoja hekaheka zetu zote na uchache tu katika kumpa sapoti tulipopigwa tulikuwa wapole.
Huu utakuwa ushindi wa 7 wa Vijender Singh kwa TKO na ushindi wa nane tangu alipoanza kuzipiga ngumi za kulipwa.
Cheka ambaye ni bingwa wa World Boxing Federation (WBF) Super Middleweight ameshashinda mapambano 32 kati ya 43 na katika ushindi huo amewatandika wengine kwa TKO mara 17 kabla ya yeye kuchomelewa leo kwa TKO.
Baada ya pambano hilo kumaliza Singh alisema Cheka alikuwa anazungumza na yeye aliamua kwamba ngumi zake ndizo zitakazoungumza
Post a Comment
Post a Comment