KIJANA mmoja amemwacha mkewe na kuamua kumuoa mkwewe mwenye umri wa miaka 42 akisema ametokea kumpenda sana.
Ndoa hiyo ilithibitishwa na mahakama.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 22 anayetambuliwa kama Matho Suraj alimwacha mkewe Latila, mwenye miaka 19  na kumuoa mkwewe Asha Devi.
Imeelezwa kuwa kitendo mapenzi hayo yaliibuka baada ya mkwe kwenda kumtembelea mwanawe kumwangalia mkwewe ambaye alikuwa anaumwa kitandani.
Wakati akimuuguza katika  kijiji cha Puraini huko Bihar,  kaskazini mashariki mwa India 2015, mtu na mkwewe wakaamua walichoamua, kuoana.
 Indian Times  imesema kwamba  Asha Devi, ambaye pia amemwacha mumewe kwa sasa anaishi na mume wa binti yake.
 Imeelezwa kuwa ndoa hiyo ilithibitishwa juni mwaka huu na mahakama.
 “Wawili hao wanapendana na hakuna sababi ya kuwatengenisha,”  mahakama iliamua.
Hata hivyo imeelezwa kuwa Suraj sasa hivi anajutia na kwamba anataka ndoa hiyo iharamishwe kwa kuwa ilikuwa ni kosa lake.
Anataka kurudiana na mkewe Latila kwa kuwa alimwacha kipumbavu.
  “Nimebaini upumbavu wangu. Nakiri kuwa nimefanyakosa lakini sitarudia tena.Simchukulii Devi kama mke wangu namtambua kama mama mkwe wangu hivyo ndivyo anavyostahili kuwa.
“Ninapiga magoti  namuomba Lalita anikubalia ili tulee mtoto wetu,”  anasema Suraj .


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO