Kim,kanye na watoto wao
MDADA Kim Kardashian kamchoka kanye West na sasa anataka talaka.
Habari zilizoifikia Us Weekly zinasema kwamba mdada huyo ambayw ameishi na Kim kama wanadoa kwa miaka miwli na nusu  sasa anataka mwanzo mpya mwakani.
Wawili hao ambaow alifunga ndoa yenye mwembwembe na ghali katika kasrui la karne ya 16 nchini Italia anataka kuachika sasa.
Wadaku wa karibu kabisa na staa huyo wameiambia Us weekly kwamba Kim Kardashian hataki kuendelea na jamaa yake huyo ambaye ameshazaa naye watoto wawili.
Binti huyo ambaye alishawahi kuolewa na  projuza Damon Thomas  na jamaa anayekipiga katika kikapu Kris Humphries, bado anatafakari kufanya hivyo ingawa bado hajampa majukumu mwanasheria wake.
 “Itachukua muda kabla hajafanya kitu chochiote kile,” alidai rafiki huyo akitafadhalisha kwamba anajaribu kutafuta sababu nzito za kulea kuhakikisha kwamba  watoto wake wawili North, 3, na Saint, ambaye ana miezi 12 wanabaki kwake.
Vinginevyo ameshaonesha kwamba hataki kuendelea na ndoa hiyo.
Tayari mdada huyo wa  Keeping Up With the Kardashians  ameshaanza kuwa mbali na mfokaji huyo wa “Fade”  mwenye umri wa miaka 39.
Tangu kutoka hospitalini Novemba 30 mwaka huu  alipokuwa akitibiwa maradhi ya akili katika hospitali ya UCLA Medical Center’s Resnick Neuropsychiatric  baada ya kukaa wodini kwa siku 9 akitibiw akitu hicho ambachow ataalamu wamekiita “temporary psychosis” — West  sasa anaendele akutibiwa kama mgonjwa wa nje.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO