WATU  wanaotafuta uwepo wa uhai katika sayari ya Mars, wamesema kwamba wamegundua uwapo wa minara mikubwa inayoashiria kwamba kulikuwa na uhai katika sayari hiyo inayofanana na dunia.

Wataalamu hao ambao hupekua taarifa na picha zinazoletwa duniani na vyombo vya Taasisi ya Utafiti wa anga za Juu ya Marekani (NASA) wamesema kwamba wameona ishara za minara mikubwa kama majengo.

Gazeti la Daily Express limeandika kuwa minara hiyo ambayo ni ya mstatiri yenye wastani wa urefu wa maili takribani moja kwenda juu inaweza kuwa ni ishara ya kuwapo kwa uhai wa aina fulani katika sayari hiyo, uhai ambao umeweza kutengeneza majengo hayo.

Ikifafanuliwa zaidi na Daily Express , imeandika kwamba wataalamu wenye kusaka uhai kutoka nje ya dunia wametengeneza nadharia nyingine kuhusiana na majengo hayo wakisema kwamba yanaonesha uwapo wa uhai au kulikuwepo na uhai.

Waatalamu hao walikuwa wanapitia picha zilizoletwa duniani na chombo cha NASA cha Mars Reconnaissance Orbiter .

Picha hizo zilikuwa zinaonesha kuwapo kwa majengo marefu sita yaliyosanjari ambayo yameitwa minara kutokana na jinsi yanavyoonekana.

Hata hivyo kuna mabishano makubwa kuhusiana na minara hiyo mitatu huku wengine wakisema ni miamba ambayo imejitengeneza kutokana na  kunyambuka kwa tabaka kunakotokana na hali ya hewa.

Mtumiaji wa YouTube anayejitambulisha kwa jina la Mundodesconocido alikuwa mtu wa kwanza kutambua majengo hayo na kusema kutokana na jinsi yalivyo huenda kabisa imetengenezwa na viumbe vyenye akili.

“Yote yanaonekana yametengenezwa vizuri hakuna hata moja linalonekana kuharibika,” aliandika Mundodesconocido. “ Itakuwa ni eneo jema kabisa kuanzisha makazi ya wanadamu katika sayari hiyo kama hayana mtu au kiumbe chochote ndani yake.”

hata hovyo wanasayansi bado wansema kwamba sayari hiyo haina viumbe hai labda wawe chini ya uso wa sayari. Na kwamba kama kuna maisha basi itakuwa viumbe hai vidogo vinavyofanana na minyoo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO