KUNA kitu na boksi kinatarajia kutua kwa watazamaji sinema Juni 2 mwaka huu. Tayari trela lake rasmi limeshaanza kutembea katika You Tube  na katika webu yake rasmi.
Hiki kitu na boksi  ni cha Gal Gadot muisrael anayeonekana kutikisa anga za sinema za aksheni kwa upande wa wanawake kutokana na muonekano wake, urembo wake na namna ambavyo anajituma katika sinema hizo.
Mdada huyu analeta kitu ambacho katika komiki kimeleta shida sana "Wonder Woman,".
Trela lake rasmi limeonwa katika tamasha la Comic-Con lililofanyika mjini San Diego, California hivi karibuni.

Katika sinema hiyo ambayo ni muziki munene, Gadot anaonekana kuwapiki kabisa wanaume katika sinema za aksheni zenye ushujaa mkubwa.
Wonder Woman mwaka huu anatimiza miaka 75 ya uchapishaji wa vitabu vyake katika muonekano mbalimbali  na safari hii Gadot amewakilisha vyema aina ya wanawake  Amazon wenye nguvu kubwa.

Gadot ni mdada mwenye nguvu kubwa ambaye uwezo wake wa kupigana si wa kawaida, kabla ya kuendelea kutawala watu wake anaenda safari ambayo ndiyo hiyo inayokuletea wewe starehe.

"Wonder Woman  ana moyo wa kibinadamu ana nguvu za kiungu na mchanganyiko wake  ndio unaotoa nguvu kubwa," anasema Gadot  akielezea arimu wake ambaye anamwakilisha.

Katika simulizi na trela lake unaona kwamba Wonder Woman  itakuwa moja ya filamu kubwa yenye hadhi ya aina yake kutokana na jinsi ilivyosukwa, ilivyosimuliwa na jinsi inavyouzwa kwa jamii kama tende wakati wa majira ya njaa.

Uchukuzaji wa picha kwa ajili ya filamu hii ulianza Novemba 2015 na kuendelea hadi Mei 2016.Wonder Woman  inatarajiwa kuachiwa katika mfumo wa 2D,3D na IMAX 3D juni 2 mwaka huu.Ikiwa imemchukua kinara katika masimulizi ya DC Comics wa jina lile lile, sinema hii itakuwa ya  nne kutolewa an  DC Extended Universe, ikisambazwa na Warner Bros. Pictures.

Filamu hii ikiongozwa na  Patty Jenkins, kuandikwa na Allan Heinberg, Geoff Johns na Patty Jenkins,  kutokana na stori inayosimuliwa na Heinberg  na mwenzake Zack Snyder, waigizaji wake ni Gal Gadot, Chris Pine, Connie Nielsen, Robin Wright, Lucy Davis, Lisa Loven Kongsli, Danny Huston, Elena Anaya, Ewen Bremner, Saïd Taghmaoui na David Thewlis.

Katika sinema hii ya Wonder Woman inaanzia  na  kuokotwa katika fukwe kwa rubani wa ndege Steve Trevor na Diana kwenye kisiwa cha Themyscira.
Rubani huyu anamsimulia Princess Diana kuhusu vita kuu ya dunia inayoendelea, anaona ni vyema kwenda kuisimamisha.

Baada ya kusimuliwa Diana anaondoka nyumbani hapo kwenda kuzuia  vita na ndipo hapo anapokuwa mwanamke asiyeeleweka anayepata jina la Wonder Woman.

Gal Gadot kama Diana Prince  ambaye ndiye  Wonder Woman, kimsingi ni mpigana vita ambaye ana nguvu za ziada zisizo za kibinadamu lakini mwishoni mwa siku ni mwanamke mwenye akili sana  na anayetibuliwa na  hali hiyo.

Mwanamke huyu  amerejeshwa miaka 100 nyuma akiwa bado mshamba na ubwawa wa shingo bado kumtokla.
 Ili aweze kumudu  nafasi hii Muisrael huyu alifanya kazi katika chakula, mazoezi mbalimbali ya kungu fu na karate na kuongezeka pauni 17 katika misuli yake.

Filamu za Wonder Woman  zilianza kutengenezwa mwaka 1996 na mpaka inatoka mambo mengi yamefanyiak waandishi wengi wameingia na kutoka na pia watengenezaji wengi wameingia na kutoka na hata waigizajiw enyewe.

Uzalishaji huu ulioanza Novemba 2015 kwa jina la uzalishaji Nightingale ulifanyika katika maeneo ya Trafalgar Square  mjini London na maeneo kadhaa uya Kusini mwa Italia kama Sassi di Matera, Castel del Monte, Palinuro na Camerota.


Matthew Jensen kama dairekta wa foto aliwapeleka wati Uingereza, Ufaransa na Italia. Kazi ya London ilimalizika Machi 13, 2016. Hukun Machi 20, 2016, upigaji filamu ulikuwa unaendelea nchini Italia na  baadae Aprili kazi hiyo ikawa inafanyika Louvre, ambako gari kubwa la Wayne Enterprises lilionekana  pamoja na Gadot. Utengenezaji wa kwenye field ulimaizika Mei 2016.

Gal Gadot-Varsano  ni myahudi aliyezaliwa Aoprili 30 1985. Yeye pamoja na kuwa muigizaji ni mmodo.
Gadot  anajulikana pia kwa uigizaji wake kama Gisele Yashar  kwenye sinema za The Fast and the Furious .
2016, Gadot alianza kucheza nafasi za Wonder Woman kwenye  DC Extended Universe,  akianzia na sinema ya Batman v Superman: Dawn of Justice na sasa yeye ndiye kinara wa Wonder Woman (2017).
Katika miaka ya karibuni alikuwa anaelezwa kama mmoja w amamodo wa Israel anayetengeneza fuba kubwa nyuma ya Bar Refaeli. Aidha yupo kwenye pafyumu ya Gucci ya Bamboo.

Akiwa amezaliwa na kukua maeneo uya Rosh HaAyin, Israel maana ya jina lake la kwanza ni wimbi na jina lake  la ukoo maana yake kingo za mto.

Yeye ni binti wa Irit (née Weiss), mwalimu na Michael Gadot, mhandisi.  Mdada huyu ana damu nyingi  zikiwamo za Poland za Kiustria, za kijerumani na za Czech.

Binti huyu amepitia jeshini na anasema miaka 3 aliyekuwapo huko ilimsaidia sana katika kazi yake ya sasa. Ilimfunza nidhamu na kujituma na kuuza uhuru wako kwa manufaa ya wengine.Akiwa na miaka 18, Gadot alishinda taji la urimbwende Miss Israel 2004.  Gadot ili aweze kutengeneza sinema ya Wonnder Woman  alilazimika kuchukua mafunza ya upanga au maarufu kama swordsmanship,  mafunzo ya Kung Fu kickboxing, capoeira  na  Brazilian jiu-jitsu

Gadot ameolewa na mtu anayetngeneza makazi na kuuza Yaron Varsano Septemba 28 2008. Na wawili hao walikuwa na hoteli ya kifahari ya Neve Tzedek iliyoko Tel Aviv, ambayo walimuuzia Roman Abramovich mwaka 2015  kwa dola za marekani milioni 26 milioni.
Wawili hao wana watoto  na mdada ni mpenzi mkubwa wa kuendesha pikipiki na  anamiliki Ducati Monster-S2R.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO