Aliyewahi kuwa Golikipa wa kutegemewa wa timu za Majimaji ya Songea,Prison na Mbeya City za Jijini Mbeya na hatimaye timu ya Kagera Sugar DAVID ABDALLAH BURHAN amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa kocha wa timu ya Kagera Sugar Meck Mexime, Burhani ameugua tumbo siku tatu zilizopita walipofika Kagera alilazwa kwenye hospitali ya Kiwandani na kuwa baadaye macho yake yalianza kubadilika na kuwa ya njano.
''Tulifanya booking ya ndege kuelekea Bugando, tulichelewa, tukapata jana amefikishwa Bugando leo asubuhi tumepata taarifa kuwa amefariki dunia'' anafahamisha Kocha Mexime.
Hata hivyo anasema kuwa hadi sasa wapo katika taharuki wachezaji wote wanalia, watajaribu kuomba shirikisho la soka liahirishe mechi zake za karibuni hadi hapo watakapomaliza mazishi ya mchezaji mwenzao.
Nimemfahamu David Burhan akiwa timu ya Prison wakati ule akiwa chini ya kocha Juma Mwambusi, baadaye Mwambusi alipohamia Mbeya City naye David Burhani akahamia timu hiyo nadhani kutokana na kocha huyo kutambua umuhimu wa golikipa huyo kwa timu yake mpya.
Chini ya golikipa David Burhan timu hiyo ilifanikiwa kufanya vyema katika ligi hiyo mwaka 2013-14 kiasi cha kushika nafasi ya nne katika ligi hiyo.
Burhani aliondoka katika timu ya Mbeya City na kujiunga na timu ya Kagera Suger hadi kifo kilipomchukua.
Inna Lillahi Waina Ilayhi Rajiuwna!!!!Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO