JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA


UTOAJI RUZUKU AWAMU YA TATU KWA WACHIMBAJI MADINI WADOGO, TAREHE 17 JANUARI 2017, MPANDA.
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) itatoa Ruzuku ya jumla ya Shilingi Bilioni 7.481 kwa Wachimbaji Madini Wadogo 59 waliokidhi vigezo vya kupata ruzuku hiyo kati ya 592 walioshindanishwa.
Hafla ya utoaji wa Ruzuku hiyo itafanyika siku ya Jumanne, tarehe 17 Januari 2017, Mjini Mpanda katika Uwanja wa Shule ya Msingi, KASHAULILI.
Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim  M. Majaliwa (Mb.).
Taarifa zaidi kuhusu  Ruzuku hiyo inapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Nishati na Madini, www.mem.go.tz na Ofisi za Madini za Kanda.
Imetolewa na,
                                                  
Prof. Justin W. Ntalikwa
KATIBU MKUU

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO