Rais wa  Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein  akikagua gwaride
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume akiteta na  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka  53 ya Mapinduzi  ya Zanzibar  zilizofanyika kwenye uwanja wa Aman Zanzibar Januari 12, 2017. 

Baadhi ya waandamanaji wakishangilia  wakati walipopita mbele ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed  Shein katika maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Zanzibar Januari 12, 2017

1A2014  Mmoja wa wananchi wa Zanzibar akimsikiliza kwa makini Rais wake, Dkt. Ali Mohammed Shein  wakati alipohutuba katika Maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwenye uwanja wa Aman Januari 17, 2017

Add captionRais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd wakifuatilia kwa makini gwaride  la Maaddhisho ya miaka 53  ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Januari 12, 2017.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi cha Zanzibar akipita   kwa ukakamavu mbele ya  mgeni rasmi Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein  katika gwaride la kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 2017

Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  wakionyesha uwezo wao wa kupigana bila silaha katika Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye wawnja wa Aman Januari 12, 2017.

Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  wakionyesha  jinsi matofari yanavyoweza kuvunjwa juu ya kichwa katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Januari 12, 2017

Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwa  amelala  juu ya misumari  huku wenzake wakipita juu yake ikiwa ni moja ya maonyesho ya ukakamavu yaliyoonyeshwa na Makomandoo hao katika maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman Januari 12. 2017.

Rais wa  Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein  akihutubia katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman   Januari 12, 2017. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO