MWANAMKE mmoja anayeishi na mume wake katika eneo la Chipata nchini Zambia na mtoto wake wa kambo anashikiliwa na polisi baada ya kumfanyia kitu mbaya mume wake katika mzozo wa malezi ya binti huyo ambaye si wa kuzaa yeye.
Imeelezwa kuwa baba huyo alipoingilia kati zogo la mtoto wake kutupwa nje  na kuumizwa, alitandikwa na kuachwa kufa.
Mke huyo aliyetambuliwa kwa jina la  Clara anadaiwa Alhamisi asubuhu alijaribu kumuua mumewe Goldwin Kamtunda baada ya kutokea kwa zogo hilo.
Imeelezwa kuwa wawili hao walikuwa wanazozana kuhusiana na jinsi mama huyo anavyomtesa binti hyuyo wa miaka mitano. Imeelezwa kuwa mama huyo alikuwa na mazoea ya kumwamsha binti huyo wa miaka mitano saa kumi na moja alfajiri afanye kazi za nyumbani na wakati mwingine alikuwa akimwamsha ili aende akkae nje wakati anatakiw akulala usingizi.
Imeelezwa janauri 12 mwanamke huyo alimwamsha mtoto  alfajiri mno akamdaka na kumtupa njne kwa nguvu kiasi ya kwamba mtoto aliumia na kuanza kulia.
Baba aliposikia sauti ya mtoto wake alimfuata kujua kuna nini na kumuuliza mkewe nini kimetokea ambapo alimjibu kihuni kwamba kwani mtoto wake ana umuhimu gani mpaka alale saa sita au saa saba na kusema kwamba hamtaki mtoto (ushe wamene uyu mwana how special is she that she can b sleeping upto 6 or 7hrs, in fact I don’t want this child here, ayende kwambuye bake, asaniteke fine ine.)
|Clara

Akaendelea kusema:Why should I be keeping kamwana koyonda monga ka mosquito. Na wakati akivurumisha maneneo hjayo akaenda kumsukuma tena mtoto yule. Mume akakasirika na kumtwanga kibao kisha akarejea ndani kujiandaa na kazi.
Wakati akitoka chumbani mwanamke alimtwanga na  kikombe kikubwa cha udongo na jamaa akaanguka chini na kupoteza fahamu. Baada ya hapo mwanamke huyo akatwa vikombe viwili vya udongo akavivunja na kuanza kumshambulia mume wake kwa kumkatakata huku akiwa amezimia.
Wakati majirani wanafika aliwaambia yeye anaondoka waende kumzika (, mutengeni uyo, napaya, go u bury him ine nayenda.) na akaondoka.

Majirani walimtwaa mume huyo aliyezimia na kumkimbiza hospitalini kwa matibabu. Taarifa zikafikishwa polisi , mwanamke huyo akasakwa na kutiwa mbaroni sasa anasubiri kufikishwa mahakamani.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO