MGANGA wa kienyeji maarufu katika jiji la Lusaka, Kalonga Kanono ametiwa mbaroni kwa kumtandika risasi dada yake.
Imeelezwa kuwa mganga huyo alimtandika risasi dada yake Josephine Chilufya ( 53) mwenye makazi Chibolya.hali ya dada huyo inaendelea vyema.
Mganga huyo matata mwenye umri wa miaka 39 ana mashauri kadhaa katika vituo vya polisi mashauri ya kutishia kuua ndugu zake.
Kalongo Kanono ambaye jina lake halisi ni Chilufya Chileya anaishi maeneo ya Kanyama .
Kwa mujibu wa ofisa uhusiano  wa Jeshi la Polisi Esther Katongo,mdada huyo amepata jeraha la risasi katika eneo la juu la mkono wa kushoto.
Taarifa zinasema kwamba  mganga huyo amekuwa na kawaida ya kutishia kuua ndugu zake zake wote.
Polisi wamesema kwamba wameitwa bastola hilo na  makasha tupu matano kutoka katika eneo la tukio.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO