Mkazi wa mtaa wa Lungo, Kata ya Kiwanja Cha Ndege , Manispaa ya Morogoro, Feithy Chibada  , akichovya kwenye wino kidole chake ikiwa ni hatua ya mwisho ya zoezi la upigaji kura katika kituo cha Lusanga -1,  kwenye  uchaguzi mdogo  uliofanyika leo kuwania nafasi ya Udiwani wa Kata hiyo.( Picha na John Nditi).
………………………
WANANCHI 10, 447 wa Kata ya Kiwanja cha Ndege ,Manispaa ya Morogoro waliojiandikisha wapigakura halali walitarajia kupiga kura  ili kumchagua Diwani wa Kata hiyo.

Uchaguzi mdogo  umefanyika leo  baada ya kutokea kwa kifo cha ghalfa cha diwani wake kupitia CCM , Godfrey Mkondya , aliyefariki miezi michache baada ya  uchaguzi mkuu wa 2015. 

Licha ya kufanyijka uchaguzi huo leo idadi ya watu waliokuwa wamejiandikisha kupiga kura  , licha ya vituo kufuguliwa kwa wakati waliokuwa wakijitokeza kwenda kupinga kura  nyakati za asubihi hadi mchana kasi yake ilikuwa ni ya kusuasua.

Mwandishi wa habari hizi alitembelea vituo kadhaa kati ya 25 vilivyopo kwenye mitaa 13 ya Kata ya Kiwanja cha Ndege , Manispaa ya Morogoro na kushuhudia  hadi  saa sita mchana vituo vingi vikiwa havina foleni ya wapiga kura na  kujitokeza  mmoja mmoja .

Msimamizi wa Kituo cha Lusanga -1 ,mtaa wa Lungo, Jennifer Rashid, alisema kuwa licha ya kufungua kituo  saa moja asubuhi, wapiga kura waliokuwa wamejitokeza walikuwa ni wachache .

Alisema,  hadi kufikia majira ya saa tano asubuhi waliojitokeza kupinga kura walikuwa 87 kati ya wapinga kura  356 walioandikishwa kwenye kituo hicho.

“ Ni mapema mmno kusema waliojitokeza kuja kupinga kura ni wachache  , tunasubiri hadi saa kumi jioni nitaweza kuona idadi halisi , lakini kwa sasa hadi  saa tano asubuhi  waliokwisha kupinga kura ni 87 kati ya 356” alisema Jennifer.

Naye Msimamizi wa kituo cha Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kiwalani-1 , Mariam Rajab , alisema kuwa muda wa asubuhi hawakupata watu wengi na walitarajia kuanzia majira ya saa nane mchana kuwapata watu  waidi kwa kuwa muda wa  mwisho wa upigaji kura ni saa kumi jioni.

Mariam , alisema hadi kufikia saa sita mchana , watu waliojitokeza kupinga kura walikuwa ni 70 kati ya wapinga kura halali  279 waliojiandikisha katika kituo hicho.

Hata hivyo baadhi ya  mawakala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ,Kituo cha kupinga kura Posta  Kiwanja cha Ndege -1 na 2 waliwazuia waandishi wa habari  kusongelea eneo hilo kupata taarifa ya zoezi hilo kutoka kwa msimamizi wa kituo.

Mawakala hayo wakidai kuwa  waandishi wa habari hawajatajwa ndani ya  kanuni za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  kuwepo katika eneo la vituo  vya   kupinga kura  hivyo hawapaswi kuwepo kwenye vituo hata baada ya kuwaoneshwa  kibari cha barua kutoka kwa Msimamizi wa Jimbo la Morogoro Mjini.

“ Hatuwataki waandishi wa habari kwenye  kituo hiki , kuchukua taarifa zetu , kwani hawapo kwenye kanuni za NEC , hivyo watupishe “ alisema walaka wa Chadema bila kujitambulisha jina lake.

Hadi kufikia majira ya saa 5: 30 asubuhi  kwenye Kituo cha Posta  Kiwanja cha Ndege -2,  watu waliokuwa wamejitokeza kupinga kura walikuwa 70 kati ya wapinga kura  331 walioandikishwa  katika kituo hicho.

Uchuguzi kwenye baadhi ya  vituo vya Kata hiyo waliokuwa wakijitokeza zaidi kupinga kura ni wanawake na wazee wa jinsia zote mbili, hali vijana wakiwa ni wachache tofauti na ilivyokuwa kwenye kipindi cha  kampeni za uchaguzi huo .

 Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Morogoro mjini, John Mgalula, alisema kuwa , vituo vya kupigia kura vipo 25 katika mitaa 13 na wapiga kura halali waliojiandikisha ni 10,447 na Vyama sita vya siasa vinashiriki katika uchaguzi huo mdogo wa Udiwani Kata ya Kiwanja cha Ndege , Manispaa ya Morogoro.

Mgalula , alivitaja  vyama hivyo na wagombea wake ni  Chama cha Mapinduzi (CCM),  mgombea wake ni Isihaka Sengo , CUF mgombe wake ni  Abeid Mlapakolo.

Vyama  vingine ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADMA ) mgombea wake ni  Salum Milindi , TLP  Julius Msilanga, Chama cha ACT- Wazaendo  ni  Rahim Elias  na  Chama cha Sauti ya Umma (SAU), mgombea ni  Mussa  Kimonje .

Uchaguzi huo mdogo  unafanyika baada ya kutokea kifo cha ghalfa cha diwani wa kata hiyo kupitia CCM , Godfrey Mkondya ,  miezi michache bada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa 2015.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO