Mshindi wa  kitita cha shilingi Milioni 30/- aliyebashiri matokeo ya mechi za ulaya kupitia M-Bet, Mkazi wa   mkoa wa Songwe,Christian Kiyeyeu(kulia)akishikwa na butwaa la kutokuamini kama yeye ndiye mshindi wa kitita hicho  wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa hundi yake na Meneja wa huduma kwa wateja wa M-bet,Jaykishan Kaba(kushoto) na Msemaji wa kampuni hiyo Gudluck Wambura mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Mwalimu wa shule ya sekondari,Wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe,Christian Kiyeyeu mwenye umri wa miaka 31 ameibuka mshindi baada ya kubashiri vyema matokeo ya mechi kupitia Kampuni ya M-Bet na kujishindia kitita cha Shilingi Milioni 30/-.

Kiyeyeu amekabidhiwa fedha zake leo katika hafla  fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za M-Bet

Kwa upande wake, Msemaji wa M-Bet, Godluck Wambura alisema kuwa Kiyeyeu alifanikiwa kuzoa kitita hicho baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi…. za ligi ya Ulaya kwa mtindo wa kucheza kawaida.

“Tumefurahi kumkabidhi mshindi wetu kitita hichi cha Sh milioni 30/- akiwa ndiye mshindi wa M-Bet ambapo amesema ataiwekeza katika biashara zake na kuweza kumalizia nyumba yake ambayo tayari alikwishaanza kuijenga,” alisema Wambura.

Aliwataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Perfect 12 na michezo mingine ni michezo mizuri inayoweza kubadilisha maisha yako mara moja ukiwa umelala masikini na kuamka tajiri kwa kutabiri kwa kiasi cha Tsh 1,000 tu unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa mchezo wa perfect 12 ambapo ukipatia zote  unaondoka na kitita chako mchana kweupe.

Naye Mshindi huyo, Christian Kiyeyeu amewashauri watanzania wote hususani walimu wenzake wenye umri unaoruhusiwa kisheria kujitokeza kubashiri matokeo ya mechi mbalimbali kupitia Kampuni ya M-Bet .

"Nashukuru sana M-Bet kwa kuniwezesha kujikwamua kimaisha, nitatumia fedha hizi kutimiza ndoto yangu ya kumalizia nyumba yangu kwa ujenzi", alisema Kiyeyeu.

Kuhusu m-Bet, ni Kampuni iliyosajiliwa chini ya Sheria za Tanzania na kupewa leseni na Bodi ya Michezo ya kubahatisha tanzania kwa lengo la kufanya upatikanaji rahisi na mwingiliano wa huduma ya mchezo wa kubahatisha (Sim Betting) nchi nzima.
Mwisho 

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO