SINTOFAHAMU ya aina yake imewakumba wafanyakazi halmshauri ya Morogoro waliohamia Mvuha kama agizo la serikali lilivyowataka baada ya kamati ya fedha na Mipango ya Baraza la Madiwani kusema shughuli zihamie maeneo mbalimbali ikiwamo Matombo.
Wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sudi Mussa Mpili akisema kwamba amri ya kuhamia Mvua inabaki palepale kama serikali kuu ilivyoagiza, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Kibena Kingo anasema hawapingi kuhamia Mvuha bali eneo halistahili kwa kukosa miundombinu.
Mwenyekiti huyo alisema  kwamba pamoja Mkurugenzi kuhamisha watu wake wote kuwa Mvuha Desemba 27, eneo hilo halikidhi  mahitaji, likiwa halina umeme na pia likiwa na nyumba chache za watumishi hali ambayo anasema itafanya  shughuli za kitawala zisifanyike.
Kibena alisema suala si kuhamisha, suala ni kama watendaji wanaweza kutoa huduma katika mazingira ya  eneo hilo.
Alisema baada ya agizo la kuhamia mvua waliitisha kikao cha kamati ya fedha na mipango ya baraza ambayo ilishauri kuwa kuwepo na mtawanyiko wa idara ili kazi ziweze kufanyika.
Alisema katika mtawanyiko wao huo, wanapeleka idara katika maeneo ya Tawa, matombo, morogoro mjini na  Mvua penyewe wakimtaka DED akakae Matombo eneo ambalo wanaona lina nyumba za kutosha na pia kuna umeme.
Hata hivyo Mkurugenzi alipozungumza na gazeti hili alisema kwamba pamoja na amari ya kuhamia hapo ipo palepale anajaribu kuelimisha madiwani hao kufuata makubaliano ya awali ya kuhamia Mvuha kama serikali kuu inavyotaka badala ya kutawanya ofisi hizo.
Alisema pamoja na kule dhiki katika utendaji, inakuwa ngumu kusimamia watendaji waluiotawanyika maeneo tofauti yenye umbali mkubwa kama madiwani hao wanavyopendekeza.
Kwa mujibu wa wafanyakazi kitendo cha kuwahamishia hapo na kuwataka woandoke kwenda maeneo mengine ni cha usumbufu mkubwa kwani ili kukwepa migongano na serikali kuu , walikubalia kuhamia hapo na wengine walishalipa kodi ya pango.
Mmoja wa wafanyakazi aliyewasiliana na gazeti hili ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema wakmba wamehamia hapo bila fedha kutoka kwa mwajiri na kutumia fedha zao kujiupatia makazi.
“hartuwezi kuelewa hili la kurejeshwa Morogoro na wengine kutawantyika maeneo mbalimbali.Tumefika hapa  wenyeji wametupatia makazi kw amalipo y ash elfu 50 kwa mwezi kwa miezi sita sasa nani atalipa hizi fedha” aliuliza mfanyakazi huyo.
Sintofahamu katika hali ambayo ilikuwa shari ya utekelezaji wa agizo  kulitokana nakikao cha desemba 30 cha kamati ya fedha ambacho kilitaka wafanyakazi kuhamia Mtamba ambako imeelezwa kuwa hakuna eneo la ofisi inayoweza kukidhi mahitaji kwa kulinganisha na Mvuha ambako yako majengo ya serikali.
Desemba 23 mwaka huu Rais alitoa tamko Mvomero akitaka watendaji kuhamia mvua na kusema wazi kwamba kama madiwani wakikataa atavunja baraza kwani  muda mrefu umepita na wananchi hawapati huduma.
Halmashauri ya Morogoro ambayo ni moja ya halamshauri za zamani  zilizoundwa wakati wa kurejeshwa kwa mamlaka za mikoa mwaka 1992 imekuwa na migongano mingi ya maeneo ya kuwekwa kwa makao makuu ya halmashauri.
Migongano hiyo ilikuwa moja ya sababu ya kumeghwa kwa wilaya ya Mvomero ambayo ilikuwa sehemu ya wilaya ya Morogoro Vijijini ambayo ipo halmashauri ya Morogoro.
Ingawa umegaji huo ulisababishwa na ukubwa wa wilaya ambayo kipindi hicho ilikuwa na kata takribani 40 mizozo ya wapi makao makuu kila diwani katika halmashauri ilirahisisha umegaji wa Mvomero.
Ingawa Mwenyekiti wa halmashauri alikana  kuwapo kwa migongano ya eneo linalostahili kuwa makao makuu, kukubali kwa Baraza katika kikao cha Desemba 26 kuhamia Mvua na , Mkurugenzi kuhamisha watu wake Desemba 27 na wao kuketi kama kamati kutoa mapendekezo mapya kunaonesha hali katika halmashauri hiyo sio shwari.
Mwenyekiti wa halmashauri alipoulizwa swali  kwamba kama ilikuwa inajulikana  Mvuha kuna tatizo kwanini hawakupendekeza  eneo jipya  katika siku za nyuma alisema yeye anayo taarifa inayoonesha tatizo la mvua lakini kwa sasa ndio wanaitisha baraza kamili kutoa maamuzi.
Alifafanua kwamba tangu awali  eneo la Mvuha limekuwa na matatizo hasa kutokana na kubainika kuwa maji yako karibu na uso wa ardhi na kwamba si sahihi kuweka makao makuu eneo hilo.
Hata hivyo hakuweza kusema kwa miaka yote hiyo tangu eneo hilo lipangwe kama makao makuu ya halmashauri kwanini hawajafanya kikao cha kushauri kubadilishwa kwa eneo.
“Sasa ndio tunataka kukaa baraza zima , baada ya mapendekezo ya Kamati, ili tupeleke mapendekezo yetu. Lakini kwa sasa tunataka, DED abaki Matombo na baadhi ya watu wengine waende maeneo mengine, Mvuha tunakwamisha utendaji wa kazi” alisisitiza.
Mwenyekiti huyo ambaye ni Diwani wa Ngerengere alisema mapendekezo yao yana maana kubwa.
Katika kuthibitisha kwamba kamati hiyo haikukurupuka, Kibena alisema kwamba alikuwa na mazungumzo na mkuu wa mkoa Kebwe Steven Kebwe ambaye aliwataka kuangalia inavyowezekana na wasikwamishe kazi za serikali na kwamba mpango huo wa ktawanya idara ameuafiki.
Juhudi za kumpata Mkuu wa mkoa kwa jana hazikuweza kufanikiwa.
Hata hivyo pamoja na kilio cha wafanyakazi ambaow amelazimika kulipa miezi sita kupata makazi wamesema wanashindwa kuelewa wafanye nini kwani tayari wengine wameshapewa taarifa na wakubwa wao kurejea katika majengo ya zamani  ya halashauri mjini Morogoro.
DED Mpili amesema kwamba  utekelezaji wa maagizo ya baraza ni mgumu kwa halmashauri hiyo yenye tarafa sita za Mvuha, Mikese, Ngerengere, Mkuyuni, Matombo na Bwakila chini.
Mimi nadhani haifai kulumbana katika hili, serikali imeagiza tutekeleze, mwenendo wa baraza unaniweka katika hali ngumu sana ya kiutawala , alisema Mpili.
“huwezi kupeleka ofisi ya Afuya Tawa, unataka Idara ikakae Tawa, huku hakuna majengo, DED akae Mvuha. Idara ya kilimo na mifugo ikakae Matombo, Utumishi na Tasaf warudi mjini; Sheria ikae Matombo hii haiwezekani” alisema Mpili na kuongeza kwamba huwezi kutawala katika utaratibu wa aina hiyo.
Kwa  mujibu wa DED makubaliano ya Kuhamia Mvuha yalifikiwa na pande zote za utawala katika kikao ambacho pia mkuu wa mkoa alikuwepo na kusema ni vyema kuanza na changamoto zingine zitaangaliwa.
Aidha kuhusu tatizo la umeme, Kibena alikiri kwamba umeme wa REA umefika tatizo ni kwamba haujawashwa na kusema kwamba makao makuu ya haklmashauri hayawezi kukaa mahali ambapo hakuna umeme na adha nyingine ikiwamo ya kukosekana kwa makazi kwa watendaji.
Pamoja na pande mbili zinazotawala  kuwa katika mazingira ya kubiashana, wafanyakazi ndio wanaokwama zaidi kwa kuwa kuna mari zaidi ya mbili katika vichwa vyao na hawajui hatima kama kufuata maelekezo ya baraza la madiwani kuhusu mfumo wap mpya wa kazi au kumfuata mwajiri ambaye wamekubaliana naye kwenda Mvuha.

 habari hii ilityoka mara ya kwanza HABARILEO

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO