Abiria watano waliokuwa katika ndege ya abiria aina ya 5H WOW ya kampuni ya Excel ya Mkoani Arusha wamenusurika kufa baada ya ndege hiyo kuanguka na kuungua moto yote.
Ndege hiyo imeanguka na kuungua moto katika eneo la sasakawa ndani ya Mbuga ya Serengeti Mkoani Mara Januari 2 mwaka huu majira ya saa 8 mchana.
 Abiria hao watano ambao bado hawajajulikana ni wa nchi gani waliokuwa katika ndege hiyo wamenusurika kufa na wako salama salimini lakini rubani wa ndege hiyo aliyetambuliwa kwa jina la Mohamedi Raza amevunjika mguu na amekimbizwa hospital Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi.
Habari kutoka ndani ya kampuni hiyo zilisema kuwa ajali hiyo ilitokea siku hiyo katika mbuga hiyo lakini abiria wote wako salama ila rubani huyo ndiye aliyevunjika mguu
 Mwandishi wa habari hizi aliyefika katika ofisi za Air Excel zilizoko uwanja mdogo wa Arusha uliopo Kisongo nje kidogo ya Jiji la Arusha kutaka kujuwa chanzo cha ajali hiyo aliambiwa kuwa msemaji wa kampuni hiyo aliyetajwa kwa jina moja la Alcado hayupo ofisini .
 ‘’Ni kweli ajali hiyo imetokea lakini Alcado ambaye ni msemaji wa kampuni hayupo na mie siwezi kusema chochote zaidi’’alisema mfanyakazi huyo aliyevaliwa nguo za kampuni hiyo ambaye aligoma kutaja jina lake.
 Gazeti hili lilipombana zaidi kwa lengo la kutaka kuonana na mmiliki wa kampuni hiyo ya ndege aliyetambuliwa kwa jina la Mike Kalaizak raia ya Ugiriki kuelezea suaka hilo aliambiwa kuwa naye hayupo ofisni amesafiri .
 Habari zaidi zilisema kuwa mbali ya Rubani wa ndege hiyo kuvunjika mguu lakini abiria wengine wote walitoka salama salami katika ajali ya ndege hiyo lakini haijajulikana kuwa abiria hao walikuwa wa nchi gani kutokana na usiri wa utoaji wa taarifa hiyo kutotakwa kutangazwa.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO