WATU kumi wameuawa katika mapigano makali ya koo baada ya koo moja kuua kijana ambaye anatakiwa kutumika katika maziko ya chifu wa koo hiyo.
Koo hizo zilizotwangana zipo Calabar katika eneo la Obubra jimbo la Cross River state.
Kwa mujibu wa Vanguard, vita kati ya watu wa Ogwurude na majirani zao Oyidah zilianza baada ay wawindaji wa Oyidah kum,uua kijana mmoja, kukata kichwa chake kwa lengo la kutumia katika maziko ya Chifu wao.
Mmoja wa mashuhuda  Clement Ekpe, alisema: “Wawindaji wa Oyidah waliotumwa kutafuta kichwa walimkimbiza kijana wa Okada ambaye alikuwa anarejea kutoka soko la Oyidah na kufanikiwa kumkamata katika maunganiko ya Ogwurude.
“Walipofanikiwa walimlazimisha binti huyo kukimbuilia katika msitu na wao wakamkata kichwa kija na Yule na kuondoka nacho.
Alisema wakati kijana huyo anauawa binti Yule alifika nyumbani kwao na kueleza kilichotokea ndipo vijana wa Ogwurude  walipokimbilia eneo waliloambiwa na kukuta mwili wa kijana huyo ukiwa hauna kichwa, ndipo walipofuatilia damu na  kufika makazi ya koo ya Oyidah .
Walipofika waliwaambia watawala wa Oyidah kuwatoa wale waliohusika na mauaji hayo ili wafikishwe polisi na waliposhindwa  kukazuka varangati la nguvu.
Mapigano hayo pia yalisababisha watu wawili kutoka Ogwurude kuuawa na nyumba kadhaa kuchomwa moto.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO