Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, akipata maelezo ya uzalishaji wa asali kutoka kwa Ofisa Misitu toka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania , Anna Lawuo  .

WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, amekitaka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia College ya Kilimo kutilia mkazi  ushirikishaji  wadau mbalimbali wakiwemo wa sekta binafsi na wataalamu wa kilimo ili kusaidia Serikali kuwa ni nchi ya  viwanda.
Mkazo huo ni katika kuwezesha matumizi ya teknolojia mbalimbali zinazopatikana katika Chuo Kikuu hicho kupitia College hiyo katika uzalishaji wa mazao ambayo yatatukika kuwa ni malighafi  katika uanzishwaji na uendelezaji wa sekta ya viwanda nchini.
Pinda ambaye pia ni mkuu wa Chuo Kikuu hicho, alitoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa sekta ya Kilimo   ambao uliandaliwa na College ya Kilimo ya Chuo Kikuu SUA.
Pamoja na mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Pinda pia uliombatana na maonesho ya zana na pembejeo za kilimo na matokeo ya mazao mbalimbali yaliyofayiwa tafiti na watafifi wa Chuo Kikuu hicho.
Pinda alisema kuwa , Rais Dk John Magufuli anayeongoza Serikali ya awamu ya tano kwa nia njema ametangaza ya  kwamba angependa  kuona nchiya Tanzania  kuwa ni ya viwanda katikakipindi cha  miaka mitano yake ya kwanza na baadaye mingine mitano kufikia miaka kumi ijayo.
Alisema kutokana na umuhimu huo ,SUA kimeazisha College ya Kilimo ambayo imejikita kwenye suala ya la utoaji wa elimu bora kwa wakulima ,uzalishaji na utafiti wa mazao na mifugo . 
 
Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, akipata  maelezo  kutoka  kwa Dk Elias Magembe ( kushoto)
Waziri mkuu Mstaafu Pinda  alisema ,Chuo Kikuu hicho kwa sasa kipo katika  nafasi nzuri  ya kuona ya kwamba kinaboresha mifumo ya kilimo  ili  wakulima waweze kuongeza uzalishaji wa mazao  yatakayowaondolea umaskini  na  upatikanaji kwa wingi malighafi  ya  sekta ya viwanda. 
“ Wataalamu wa SUA hasa wa College hii ya Kilimo mna wajibu mkubwa wa kushirikiana na wadau  sekta binafsi  na serikali katika kuhakikisha ni namna gani wanaisaidia  nchi yetu kutimiza azma yake ya kuwa ni nchi  viwanda ndani ya uongozi wa Rais wetu ” alisema Pinda.
Hata hivyo alisema , kilimo ni neno pana kulingana na fafsiri ya Shirika la Chakula Duniani  kuwa  kina jumuisha uzalishaji katika ufugaji  nyuki, kilimo cha mazao ya chakula na biashara, misitu , uvuvi na mifugo.
Alisema  kupitia College hiyo ni vyema wataalamu wake wanapaswa  kujipanga vizuri  kuwashirikisha wakulima kuwapa elimu na mafunzo bora ili uzalishaji wao uweze kuzingatia upatikanaji wa tija sambamba na ufugaji bora ambao lengo lake ni kusaidia ukuaji wa sekta ya viwanda .
Naye Mkuu wa College ya Kilimo ( Principal Colleg Of Agriculture ) Profesa Sudan Nchimbi  alisema wajibu wa Chuo Kikuu hicho ni kufundisha wataalamu  na kufanya tafiti mbalimbali zitakazo saidia wakulima kuboresha uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali  na mifugo.
Alisema , kutokana na azma hiyo, SUA imetoa wataalamu wa aina mbalimbali wakiwemo wa kilimo na kuweza kuajiriwa Serikalini na taasisi binafsi huku wengine wakiwa wamejiajiri wao wenyewe katika sekta ya kilimo na ufugaji.
 
Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, akipata  maelezo  kutoka  kwa mmoja wa wataalamu wa masuala ya ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa , Frank Mlingi 
Profesa Nchimbi alisema , Sua imeamua kuitisha mkutano wa siku mbili na kufanya maoenesho ya zana za kilimo , matokeo ya shughuli za kitafiti kwa ajili ya kupadirishana uzoezi wa kitaalam na kiuongozi kwa lengo la kuunganisha nguvu za pamoja  katika uboreshaji wa mazao ya kilimo , ufugaji na uvuni ambayo itadaidia kuboresha pia sekta ya viwanda.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha Uhandisi na Teknolojia katika utafiti wa kutumia ndege zisizo na rubani kutoka kwenye College hiyo, Profesa Boniface Mbilinyi alisema kuwa Chuo Kikuu hicho kwa sasa kimeboresha utaratibu katika masuala ya utafiti ambao ni shirikishi ili kuondoa kero zilizokuwa znajitokeza .
Profesa Mbilinyi alisema , ushirikishaji huo tangu mazo hadi mwishi katika ukusanyaji wa takwimu  za utafiti ili matokeo ya utafiti huo yaweze kufanyiwa kazi na makundi mbalimbali kwa lengo la uboreshaji wa sekta ya kilimo na ufugaji.
Source: John Nditi

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO