MVUA kubwa iliyoambatana na radi  iliyonyesha jana  majira saa tisa mchana katika kijiji cha Mibikimitali, kata ya Ifunda wilayani Iringa imeua watu wawili na wengine wanne kujeruhiwa.

Taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela imesema watu hao walikufa kw akupigwa na radi.

Kasesela alisema radi hiyo iliyopiga katika shule ya msingi Mibikimitali, iliua mwanafunzi wa darasa la nne wa shule hiyo, Goodlove Luhaga (9) na binti aliyetambulika kwa jina moja la Kulwa mtumishi wa ndani wa mmoja wa walimu wa shule hiyo aliyekuwa akikinga maji.

Kasesela aliwataja waliojeruhiwa na radi hiyo kuwa ni pamoja na Noah Mdotta (12) aliyeungua paji la uso.Wengine kwa mujibu wa mkuu wa wilaya huyo ni Frida Kibiki (13), Zela Chaula(13) na Recho Mdemu (10).


Alisema majeruhi hao walipata huduma katika kituo cha afya cha Ifunda kabla ya kuhamishiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, mjini Iringa kwa matibabu na uangalizi wa karibu.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO