Kiongozi wa upinzani wa muda mrefu nchini Kongo ya DRC, Etienne Tshisekedi, amefariki  akiwa na umri wa miaka 84.
Kiongozi huyo anayetambuliwa kwa kupigania demokrasia nchini mwake, kifo chake kimetokea mjini Brussels, Ubelgiji jana Jumatano, wakati alipoenda kwa ajili ya ukaguzi wa afya yake.
Tshisekedi alikabiliana na  Mobutu Sese Seko, kwa miaka kadhaa , hadi alipoangushwa na majeshi ya nchi tatu ya kimataifa. Aidha alikuwa mpinzani wa Laurent Kabila, ambaye alitwaa madaraka 1997, na mwanae Joseph Kabila aliyeanza kutawala kuanzia mwaka 2001.
Tshisekedi aliwahi kuwa waziri katika serikali ya Mobutu kabla ya kuanzisha Union for Democracy and Social Progress party (UDPS) mwaka 1982.
Alitajwa mara nne kuwa waziri mkuu katika mwaka 1990 lakini alikuwa akitemwa mara kadha na Mobutu.
Alitarajiwa kuchukua nafasi kubwa uongozi katika serikali ya mpito wakati Kabila anaachia madaraka mwaka huu.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO