UMOJA WA ULAYA WASAIDIA MRADI WA LISHE NA USALAMA WA CHAKULA WA WFP KATIKA MIKOA YA KANDA YA KATI, TANZANIA

                 Bw. Michael Dunford Mwakilishhi wa WFP nchini Tanzania (kulia) na Mhe. Bw. Roeland Van De Geer, Balozi wa Umoja wa ...



                
Bw. Michael Dunford Mwakilishhi wa WFP nchini Tanzania (kulia) na Mhe. Bw. Roeland Van De Geer, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania wakisaini mkataba wa makubaliano wenye thamani ya Euro milioni 9.5 kama mchango wa EU kutika kuimarisha usalama wa chakula na lishe katika mikoa ya Dodoma na Singida. Mchango huo wa EU ulitangazwa jana katika hafla ya kutiliana saini iliyofanyika kwenye jengo la Umoja jijini Dar es Salaam, ambapo Dk. Mpoki Ulisubisya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto alikuwa mgeni rasmi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula  Dunini (WFP) limepokea mchango wa Euro (€) milioni 9.5 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kwa lengo la kuunga mkono Mradi wenye thamani ya Euro milioni 24.5 (takribani Shilingi za Tanzania bilioni 50) wa kusaidia kukuza Usalama wa Chakula na Lishe katika mikoa ya kati nchini Tanzania.
Mradi umeandaliwa ili kuimarisha usalama wa chakula na lishe kwa watu wapatao 40,000  na wakati huohuo ukichangia katika kupunguza utapiamlo katika wilaya zinazolengwa za Bahi na Chamwino mkoani Dodoma na Ikungi na Singida Vijijini katika mkoa wa Singida.
Mchango wa EU ulitangazwa leo wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano katika Jengo la Umoja jijini Dar es Salaam uliofanywa na Dr. Mpoki Ulisubisya, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael Dunford, Mwakilishi wa WFP nchini Tanzania na Roeland Van De Geer, Mkuu wa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.
“Licha ya kuimarika kwa viashiria vingi vya afya katika muongo uliopita, bado hakuna hatua kubwa katika kuimarisha hali ya lishe ya watoto na wanawake nchini Tanzania,” Roeland Van De Geer, Mkuu wa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, alisema wakati wa hafla hiyo. “Viwango vya juu vya kudumaa, kukosa uzito wa kuridhisha na upungufu wa viinilishe nchini kunaashiria dharura ya kimyakimya. Utayari wa kisiasa katika safu ya viongozi wa juu katika kukabili lishe duni nchini Tanzania kwa mtazamo wa sekta nyingi kwa hakika ni mageuzi makubwa. Kupitia mradi huu, EU pamoja na WFP ziko katika nafasi nzuri ya kubaini na kuunga mkono uhusiano kati ya kilimo, afya, usalama wa chakula na lishe, ambao hapo kabla haukuwa umeelezwa kwa kina au kufuatiliwa kikamilifu.”
Mradi huu unatumia uwepo wa muda mrefu wa WFP katika mikoa ya kati nchini Tanzania na uzoefu wake katika kutoa chakula chenye lishe na mawasiliano yenye lengo la kubadilisha tabia ya kijamii kupitia vituo vya afya. Shughuli hizi zitakamilishwa na jitihada katika sekta nyingine ili kutoa mtazamo ulio kamili zaidi wa kupunguza kudumaa nchini. Viwango vya Taifa vya kudumaa viko katika asilimia 34 ambapo kwa Dodoma ni asilimia 36.5 na Singida ni asilimia 29.2
“Tunashukuru kwa mchango huu kutoka Umoja wa Ulaya kwani umeiwezesha WFP kuendelea na programu hii bunifu inayolenga kukidhi mahitaji ya watu walio hatarini zaidi, hasa watoto katika kile kipindi muhimu sana cha ukuaji wao, yaani siku 1,000 za mwanzo tangu kubebwa mimba hadi kutimiza miaka miwili,” Mwakilishi wa WFP Michael Dunford alisema katika hafla hiyo. “Programu hii itatoa ushahidi ambao utatoa mwongozo kwa jitihada za baadaye, na kwa hiyo ina uwezekano wa kuleta mabadiliko ya kudumu nchini Tanzania.”
Nchini Tanzania, viwango vya utapiamlo sugu miongoni mwa watoto unatokana na umaskini, ukosefu wa usalama wa chakula na ukosefu wa chakula cha kutosha kwa watoto wachanga na unyonyeshaji watoto. Mradi utalenga kukuza maarifa kuhusu lishe, mtawanyiko wa lishe na taratibu za kutumia maji, usafi wa mazingira na usafi wa mwili (WASH). Shughuli hizi zitapewa nguvu kwa kuhamasisha ufugaji wa idadi inayofaa ya mifugo, kupanda mazao tofautitofauti na kuhamasisha vijiji kuanzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopa, yote yakilenga kukuza uwezekano wa kupata mtaji.
Shirika la Save the Children ni mshirika wa WFP katika kuimarisha ushirikiano na uwezo wa asasi zilizojikita katika jamii ili kuhamasisha uwezeshaji wa jinsia na uhusiano wa sekta mbalimbali katika suala la lishe, pamoja na kuratibu utekelezaji wa kipengele cha kilimo katika mradi.
Kwa kuratibu shughuli hizi chini ya mwamvuli wa WFP, Umoja wa Ulaya na Shirika la Save the Children zitakuwa zikishughulikia changamoto nyingi zinazolenga kuimarisha usalama wa chakula na lishe nchini Tanzania.
Mradi huu ni sehemu ya majukumu ya WFP katika kufanikisha Lengo la 2 katika Malengo ya Maendeleo Endelevu: Kufuta Njaa. Ili Kuondoa Njaa kabisa ifikapo mwaka 2030, WFP inashirikiana na washirika mbalimbali kama vile serikali, sekta binafsi na vyama vya kiraia.
#                      #                      #
WFP ni shirika kubwa zaidi duniani la misaada ya kiutu linalopiga vita njaa duniani kote, kutoa msaada wa chakula katika maeneo ya dharura na linaloshirikiana na jamii ili kuimarisha lishe na kujenga uwezo wa kujinusuru. Kila mwaka, WFP linawasaidia takribani watu milioni 80 kote duniani katika nchi zipatazo 80.

Tufuate katika Twitter:
Shirika la Mpango wa Chakula: @WFP_Tanzania and @WFP_Media
Umoja wa Ulaya: @EUinTZ and @EuropeAid

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:  
Fizza Moloo, WFP/Dar es Salaam, Simu. +255 (0) 692 274 729 or +255 (0) 784 720 022,
fizza.moloo@wfp.org
Susanne Mbise, Umoja wa Ulaya, Ofisa Habari & Mawasiliano, +255 (0) 754 323 245,
            susanne.mbise@eeas.europa.eu

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: UMOJA WA ULAYA WASAIDIA MRADI WA LISHE NA USALAMA WA CHAKULA WA WFP KATIKA MIKOA YA KANDA YA KATI, TANZANIA
UMOJA WA ULAYA WASAIDIA MRADI WA LISHE NA USALAMA WA CHAKULA WA WFP KATIKA MIKOA YA KANDA YA KATI, TANZANIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqvbb0nka6CVfiVUlEhFqTGcSV2h6qSp0b6Ybsdn2-8lmZ3Sb8WT1ziCBgwsZD2c1jKWnKyvnyECpItx9M1kjMzictcOQiLx3OQPza6WDoBXs6HZ3G5BXexdl19x_y5dFCyvCwbL7QLG8/s320/Courtesy+of+WFP+3.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqvbb0nka6CVfiVUlEhFqTGcSV2h6qSp0b6Ybsdn2-8lmZ3Sb8WT1ziCBgwsZD2c1jKWnKyvnyECpItx9M1kjMzictcOQiLx3OQPza6WDoBXs6HZ3G5BXexdl19x_y5dFCyvCwbL7QLG8/s72-c/Courtesy+of+WFP+3.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2017/02/umoja-wa-ulaya-wasaidia-mradi-wa-lishe.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2017/02/umoja-wa-ulaya-wasaidia-mradi-wa-lishe.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy