Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akizungumza na waombolezaji .
MKUU wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri  jana aliongoza umati mkubwa wa watu kwenye maziko ya watu wanne, watatu wa familia moja  waliokufa kwa kusombwa na maji ya mvua katika kijiji cha Isighu wilayani hapa. 
Watu hao walikutwa na maji hayo baada ya mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamkia Januari 31.Mvua hiyo ilisababisha kuwepo na mafuriko yaliyosomba nyumba waliyolala watu hao.
 Waliozikwa jana ni Maritha Mabula (66) Shukuru Donard Chinyanya (15) mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari  Mwana kianga ,na Benadeta  Mabula (7) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Ilolo na mwingine ni Jeska Lubeleje (19)  mkazi wa kijiji cha  Chinyika kata ya Vighawe.
Katika maziko hayo watu waliojawa na simanzi walishindwa kujizuia na  kufikika hatua wengine kuanguka na kuzimia kwa uchungu wakati maiti hao walipowasili kutoka mochwari ya Hospitali ya Benjamin Mkapa. 
Zaidi ya watu  7 walidondoka kwa wakati  tofauti  na kukimbizwa katika hospitali ya benjamini Mkapa wilayani hapa.
Shekimweri ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya akizungumza katika maziko hayo pamoja na kutoa pole aliwataka wananchi kuhama maeneo ya hatari. 
Aidha alitaka wananchi kutunza mazingira kwani sehemu kubwa ya wilaya hiyo imeharibiwa na hivyo kufanya maji kutokuwa katika msimamo wake wa asili. 
 
Wakazi wa kijiji cha Isighu  wakimsikiliza mkuu wa wilaya akitoa nasaha kuhusiana na maafa ya maji yaliyosababisha watu wanne kufa , watatu wakiwa wa familia moja katika kijiji can Isighu, Mpwapwa.
Alisema serikali   imetoa baadhi ya gharama za maziko ikiwa ni pamoja na majeneza, mafuta na nguo ya kuzikia (sanda). 
Aidha  Shekimweri aliwataka wananchi wa  kitongoji hicho kuhama katika maeneo  hatarishi  kutokana na mvua zinazo endelea  kunyesha kwa sasa.
Alisema uharibifu  mkubwa wa mazingira  katika vilele vya milima imesababisha maji kushuka kwa nguvu bila kuwa na kinga  na hivyo kuingia katika makazi ya watu.
Watoto wawili Beka  Mlami (10) na  Joseph Sumisumi walinusurika kifo na  kujeruhiwa kwenye  tukio  hilo  la kutisha.
Akielezea tukio hilo mmoja watoto walivyonusurika na kifo  Beca  Mrami (10) alisema mara baada ya mvua kuanza kunyesha   maji yalianza kuingiandani ndipo walipo panda kwenye dari la nyumba na maji walipozidi waliamua kukimbia  na kuwaacha bibi yake na dada zake   ndani.
"Mimi nilipoona  maji yanazidi nikawaambia tukimbie bibi na akina dadawakabaki ndani  na Mandili (Joseph Sumisumi ) nilipanda juu ya paabaada ya nyumba kuanguka  nilikimbia na kuwaacha ndani"aliongea mtoto
huyo.

Source:
Sifa Lubasi, Mpwapwa

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO