https://4.bp.blogspot.com/-Veo8jQgUo8E/WMqqpps9MMI/AAAAAAAAC5k/jr7qn4IWRLQlCiwr1mM6A-I4Y1Vu_4mRACLcB/s1600/IMG_20170315_132956.jpg" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://4.bp.blogspot.com/-Veo8jQgUo8E/WMqqpps9MMI/AAAAAAAAC5k/jr7qn4IWRLQlCiwr1mM6A-I4Y1Vu_4mRACLcB/s640/IMG_20170315_132956.jpg
" width="640" />

Mgeni rasmi katika maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu Pius Chale alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga kwa
kutimiza miaka 50 pamoja na kuzindua jarida maalum la kikosi hicho akiwa amelishika linaitwa Uhodari.

https://4.bp.blogspot.com/-cOJLeZ03syk/WMqqfMvfdRI/AAAAAAAAC5Y/_J3SeGGfhYU8Ep6iIxNZHojX0EN8Jz03QCLcB/s1600/IMG_20170315_121545.jpg" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://4.bp.blogspot.com/-cOJLeZ03syk/WMqqfMvfdRI/AAAAAAAAC5Y/_J3SeGGfhYU8Ep6iIxNZHojX0EN8Jz03QCLcB/s640/IMG_20170315_121545.jpg
" width="640" />

Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha 841kj wakionyesha ukakamavu wake kwa kushindana kuvuta kamba ikiwa na lengo la kuburudisha wakati wa sherehe za miaka 50 ya kikosi cha 841kj

https://4.bp.blogspot.com/-KChR_94z6go/WMqqiT1X2sI/AAAAAAAAC5c/HWZR4K6T9ygQuQzET-oqNYTg69KYkqUvACLcB/s1600/IMG_20170315_112753.jpg" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://4.bp.blogspot.com/-KChR_94z6go/WMqqiT1X2sI/AAAAAAAAC5c/HWZR4K6T9ygQuQzET-oqNYTg69KYkqUvACLcB/s640/IMG_20170315_112753.jpg
" width="640" />

Baadhi ya vijana waliopo kwenye mafunzo ya awali ya kijeshi maarufu kama operation Magufuli kujitolea katika kikosi cha 841kj mafinga nao walikuwa miongoni mwa waliosherekea miaka 50 ya kikosi hicho.

https://2.bp.blogspot.com/-56eQaG4X4bk/WMqqtcl6VTI/AAAAAAAAC5o/zVPfnDvVtKYxMjRcYXN7soGWtnYbvF6-QCLcB/s1600/IMG_20170315_154524.jpg" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://2.bp.blogspot.com/-56eQaG4X4bk/WMqqtcl6VTI/AAAAAAAAC5o/zVPfnDvVtKYxMjRcYXN7soGWtnYbvF6-QCLcB/s640/IMG_20170315_154524.jpg
" width="640" />

Hili ndio jengo linalojengwa kwa ajili ya kiwanda cha Kukoboa na kusaga
nafaka
za kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga.

Na Fredy Mgunda,Mafinga

Kikosi cha jeshi la kujenga
taifa 841kj mafinga kimeanzisha kiwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao
wanayozalisha lengo likiwa ni kuhakikisha jeshi hilo linajilisha na kupata
mahitaji mengine kupitia uzalishaji mali.

Akizungumza kaimu kamanda wa
kikosi cha 841 kj mafinga Captain Victor Nkya katika maadhimisho ya miaka 50
tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 15 / 03 / 1967 kikiwa na lengo la kuendelea
kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli
kuwa na serikali ya viwanda kwa kuanza kujenga kiwanda cha nafaka na mifugo
ambacho kitatoa ajira wa watu wengi na kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla pamoja
na kuimalisha ulinzi kutokana na majukumu waliyonayo.

Nkya alisema kuwa kikosi cha 841kj kj mafinga
kimeamua kujenga kiwanda hicho ambacho kitakuwa kinaendeshwa kibiashara ili
kukuza ajira na pato la taifa.

“Hapa kikosini tunalima na
kufuga mifugo ya aina mbalimbali kwa wingi na kwa kiwango kinachotakiwa  kukidhi soko ili kuonyesha kuwa kikosi cha
jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga kinakuwa mfano wa kuigwa na kukidhi haja
ya kuanzishwa kwa kikosi hicho”.alisema Nkya

Captain Nkya alisema Sasa
hivi Jeshi la kujenga taifa kikosi cha 841kj kimekuwa kikosi cha Kisasa
nachenye wasomi wengi wanaweza kusaidia kubuni vitu vingi vyenye faida ya
kulisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo yake kama Kulinda Mipaka ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na kujitoa katika shughuli nyingine za kijamii.

“Tumefungua kiwanda ni
lazima sasa kuongeza uzalishaji kwa lengo la kuja kuipunguzia serikali gharama
za kukihudumia kikosi cha 841kj mafinga ukiangalia tunaeneo kubwa na tunanguvu
kazi hivyo ni lazima tulime na kufuga kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr John Pombe Magufuli anataka jeshi la kujenga taifa lirudi
kujitegemea”.alisema Nkya

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu Pius Chale alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga kwa
kutimiza miaka 50 kwa kuwa kudumu huko kwa kikosi hicho ni hatua kubwa sana
katika ujenzi wa taifa.

Chale alikitaka kikosi cha
841kj kurudisha uzalendo kama zamani ili kuendelea kuzalisha chakula kwa wingi
kama zamani kwa saizi kikosi hicho kin
alima eneo dogo sana kitu kinachochangia kuipa serikali wakati mgumu wa
kikihudumia kikosi hicho.

“Nimetembea eneo kubwa sana
leo lakini nimeona eneo la uzalishaji ni dogo sana hivyo mnahitaji kuongeza
uzalishaji ili kuisadia serikali kuzalisha chakula kwa wingi nyie mna nguvu
kazi hapa lakini bado sijaona mkiitumia ipasavyo”.alisema Chale

Aidha Chale alikipongeza
kikosi hicho cha 841kj mafinga kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kuanza ujenzi wa kiwanda ambacho
kitaongeza ajira,uzalishaji wa bidhaa za chakula na kukuza uchumi wa nchi
kutokana na uzalishaji wake.

“Nichukue fursa hii
kuwapongeza kwa kuweza kuwa na wazo zuri kama hili la kujenga kiwanda hapo ndio
mnakuwa mnatimiza malengo ya kikosi cha 841kj mafinga kwa kukuza uzalishaji kwa
kutumia raslimali watu ambao mnao katika kiosi kuzalisha na sio kila siku
mnakuwa mnategemea msaada kutoka serikalini”alisma Chale

Chale alikitaka kikosi
kuendelea kutunza nidhamu waliyonayo na kuendelea kumuunga mkono Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli katika jitihada zake za
kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi na viwanda.

Naye Bwana shamba
wakikosi (farm manager)
luteni Francis Breek wa kikosi cha 841kj alisema
kuwa wamejipanga kuongeza uzalishaji kwa kuwa wana eneo kubwa na wana wataalamu
wengi wanaoweza kukidhi mahitaji ya kukuza uzalishaji.

“Ukiangalia mwaka huu
tumelima eneo kubwa na tumeongeza idadi ya mifugo hivyo tunatarajia kuongeza
tena idadi ya mifugo na kupanua eneo la kilimo ili kuongeza uzalishaji kwa kuwa
tumejenga kiwanda na kiwanda kinahitaji uzalishaji mkubwa wa nafaka pamoja na
ufugaji mkubwa na wenye tija”alisema Breek

Lakini pia kikosi hicho cha
841kj Mafinga kilizindua jarida linaloitwa uhodari ambalo linaonesha kila kitu kinachofanywa na
kilichofanywa na kikosi hichotoka kuanzishwa kwake.

“Hongera kikosi cha 841kj
kwa Kutimiza Miaka 50 Tokea Kuanzishwa kwake”

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO