Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (wa pili kushoto)  na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako kwa pamoja  wakizindua Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda.
KATIKA ushindani wa utoaji wa huduma za simu kwa wateja nchini,Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  Tanzania leo imezindua ofa itakayowawezesha wateja wake wote nchini kuongea bila kikomo mara tu baada ya kujiunga.
Ofa hiyo ambayo imetambuliwa kama “Airtel HATUPIMI Bando” itapatikana katika  vifurushi mbalimbali ikiwemo kifurushi cha  siku, wiki na mwezi.
Aidha vifurushi hivyo vimesheheni  dakika zisiso na kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuzungumza bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi.
Akizungumzaa wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo,  Mkurugenzi wa Masoko, Isack Nchunda alisema: “ Airtel Hatupimi, sasa Hatupimi dakika zenu za maongezi, tunaleta huduma hizi nafuu kwa kuwa tunaamini katika kuendelea kuboresha huduma zetu  ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa  kuwapatia thamani ya pesa zao katika huduma na bidhaa zetu.”
“HATUPIMI Bando”  ina vifurushi vya Hatupimi kwa siku vya hadi 1000/= pia vipo vya wiki kwa shilingi 5000, na vilevile unaweza kujiunga na HATUPIMI kwa mwezi kwa shilingi 10,000/= .

Airtel imekuja  na ofa yake ya hatupimi siku chache tu baada ya kuzindua ofa kabambe kupitia huduma ya Airtel Money, Vile vile airtel wiki hii ilizindua kampeni ya kufungua maduka yake 2,000 yatakayotoa huduma kwa wateja ili kuwafikishia wateja wake wote huduma zao popote walipo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO