UKIINGIA kwenye sosho media unakutana na kelele nyingi za kumtaka kaka Paul Makonda aoneshe  vyeti vyake na jina lake la ukweli, kelele ambazo mwenye kigoda kasema hazina tija na kumtaka Paul Makonda kuendelea kuchapakazi.

Wakati nyumbani Tanzania kunatokea hayo ya mtandao, leo nchini Nigeria nako kuna kasheshe la namna hiyo lakini wenzetu wao wameunda tume kuchunguza ukweli kuwa seneta mmoja(watunga sheria hawa, wabunge) kasema uongo kuhusu chuo kikuu alichoenda na kwamba amegushi cheti.

Ndio kusema baraza la seneti la Nigeria limetaka uchunguzi ufanywe dhidi ya seneta mwenzao Melaye kuhusu uhalali wa vyeti vyake.

Taarifa iliyofikia  blogu hii saa moja iliyopita inasema kwamba Baraza la seneti la Nigeria limeanzisha uchunguzi rasmi  dhidi ya  seneta Dino Melaye kwamba amefoji (kugushi) vyeti alivyotumia kuwania nafasi hiyo ya utungaji wa sheria.

Uchunguzi huo ulianzishwa baada ya hoja binafsi ya seneta Ali Ndume anayewasilisha jimbo la Borno South ambaye alitaka  seneta huyo na mwingine kuchunguzwa ili ibainike ukweli wa jambo hilo.

Kwa mujibu wa Ndume,  Melaye hakupata digirii ya chuo kikuu cha Ahmadu Bello University (ABU) kilichopo Zaria kama alivyodai kwenye wasifu wake (CV).

Tume iliyoundwa inatarajiw akukamilisha kazi yake katika kipindi cha wiki mbili bna kuiwaikilisha katika baraza hilo kwa maamuzi.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO