RIPOTI ya shirika la Chakula duniani (FAO) inasema asilimia 15 ya samaki wanaovuliwa duniani ambao ni sawa na tani Milioni 26 wanatokana na uvuvi haramu na hivyo kuleta tishio kwa uendelevu wa rasilimali za bahari na uhakika wa chakula.

Taarifa hiyo inazitaja nchi za Afrika Magharibi ikiwemo Guinea, Siera Leone, Morroco, Mauritania na Angola kuwa ni mataifa yaliyoshamiri vitendo vya uvuvi haramu kukiwa na idadi kubwa ya meli na makampuni yanayojihusisha na uvuvi haramu zinapofanya safari za majini.

Aidha utafiti uliofanywa na chombo cha Umoja wa Ulaya kilichoanzishwa kusaidia nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (CTA) unaonyesha kuwa  jumla ya hasara ya sasa inayotokana na uvuvi haramu duniani kote inakadiriwa kuwa kati ya dola bilioni tisa na 24 kwa mwaka.

Nchi zinazoendelea zipo hatarini zaidi kukumbwa na uvuvi haramu, huku jumla ya samaki wanaovuliwa kwa njia haramu katika Afrika Magharibi pekee ikifikia hadi juu ya asilimia 40 kuliko samaki wanaoripotiwa.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo mwaka 2016 FAO iliandaa mkataba wa kimataifa kuhusu udhibiti wa uvuvi haramu ambao tayari umeridhiwa na nchi 30 na hivyo kuanza kutumika kisheria, ambapo unalazimisha nchi wanachama kuhakikisha boti zote zinazoingia bandarini nchini mwao zinaheshimu kanuni za uvuvi endelevu.

Tanzania kama zilivyo nchi nyingine zilizopo katika ukanda wa bahari, mito na maziwa imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za mashirika ya kimataifa katika kupiga vita tatizo la uvuvi haramu, ambao unaendelea kuathiri mazalia ya samaki sambamba na uchafuzi wa mazingira ya bahari.

Uvuvi haramu unatajwa kushamiri zaidi katika maeneo mengi ya pwani kuanzia Dar es Salaam, Mtwara hadi Tanga, hatua inayoisababishia Serikali kukosa mapato ya fedha za kigeni pamoja na kudumaza mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inasema sekta ya uvuvi inachangia asilimia 2.4 yapato la taifa wakati ukuaji wake ni wa kiwango cha asilimia 5.5 kwa mwaka na kutoa ajira ya kudumu kwa wavuvi 185,000.

Pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuwahimiza wavuvi kuzingatia sharia, kanuni na taratibu zilizopo, baadhi ya wavuvi wamekuwa wakitumia zana na vifaa vya uvuvi zisivyo rasmi ikiwemo nyavu, matumizi ya mabomu ya sumu na hivyo kupelekea tishio la kupotea kwa rasilimali hizo muhimu.

Hivi karibuni Serikali ilitangaza operesheni maalum kwa kuunda kikosi kazi maalum kinachojumuisha Wizara saba ikiwa ni mkakati maalum wa kupambana vikali na wavuvi haramu pamoja na waigizaji, wauzaji na watumiaji wa zana zisizoruhusiwa katika uvuvi.

Kikosi kazi hicho kinahusisha Wizara mbalimbali ikiwemo OfisiyaRais- TAMISEMI, Ofisi ya Makamu waRais-Mazingira, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa, Wizara ya Mambo  ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Kilimo,  Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Maliasili na Utalii, na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea soko la kimataifa la samaki lililopo Feri Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Kilimo, Mifugo naUvuvi, Dkt. Charles Tizeba alisema hakuna namna nyingine ya kukabiliana na vitendo hivyo haramu zaidi ya kuweka adhabu kali kwa wanaotiwa hatiani.

“Baadhi ya makosa ya uvuvi haramu kuwa ni uhujumu uchumi au ugaidi wa silaha (terrorism) kwa vile wanatumia milipuko  au mabomu na kumaliza mazalio ya samaki na kutishia wafanyakazi wa Serikali wanaofuatilia masuala hayo” anasema Dkt. Tizeba.

Kwa mujibuwaDkt. Tizeba anasema Serikali imebaini mapungufu yaliopo katika  sheria zilizopo, hivyo imejipanga kuwasilisha mabadiliko Bungeni  ambapo, itaamuliwa  kwa kiasi gani wataweza kuwabana wavuvi walio waharibifu na wavunjaji sheria.

Anasema sekta ya uvuvi nchini inatawaliwa na sheria kuu mbili za Sheria ya Uvuvi ya mwaka 2003 na Sheria ya Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka 2009, ambazo hazimfanyi mtu kuacha uvuvi haramu lakini iwapo adhabu itaongezwa, wengi wataogopa.

Anaongeza kuwa mikakati hiyo ya Serikali imekuja baada ya sheria na kanuni zilizopo kushindwa kupambana kikamilifu na vitendo vya uvuvi haramu vinavyotishia ukuaji wa sekta ya uvuvi nchini.

Aidha anasema Serikali itafanya mabadiliko ya sheria zinazosimamia uvuvi kwa kuyaainisha baadhi ya makosa ya uvuvi haramu kuwa ni ya uhujumu uchumi, ili kuongeza adhabu iwe kali kwa watu wanaotiwa hatiani kwa makosa hayo.

Waziri Tizeba anaongeza kuwa Serikali inaendelea na operesheni zake za kudhibiti uvuvi haramu katika mnyororo wote wa thamani kwa maana kutoka kwa watengenezaji zana haramu, wanaoziingiza nchini, wasafirishaji na wavuvi.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Yohana Budeba anasema Serikali imenunua boti nane za kisasa zenye thamani ya Tsh. Milioini 640 kwa ajili ya kuongeza nguvu ya doria na kupambana na uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali ya uvuvi nchini ikiwemo maziwa makuu ya Victoria, Nyasa na Tanganyika.

Dkt. Yohana Budeba anasema boti nne kati ya hizo zimenunuliwa nchini Afrika Kusini na nyingine zinaendelea kutengenezwa hapa nchini katika kituo cha kunduchi ikiwa ni jitihada za Serikali za kukabiliana na Uvuvi haramu ambao umeanza kutishia kutoweka kwa baadhi ya samaki katika Mito, MaziwanaMabwawanchini.

KuhusuuvuviwasamakikatikamajiyabahariKuu, Dkt. Budeba anasema Serikali imeanzisha kituo cha udhibiti wa uvuvi kwenye maji ya kina kirefu cha bahari kuu ambacho kitasaidia nyendo za vyombo vya uvuvi wakiwemo wavuvi wa kimataifa wanaoingia kuvua samaki kinyume cha sharia na taratibu za nchi.

Mazao ya samaki pamoja na kuwa kuchanzo cha kipato kwa watanzania wengine na taifa kwa ujumla, lakini pia samaki wanachangia katika kuwapatia lishe na kwa sababu hiyo matumizi endelevu ya mazao ya bahari na bahari ni jambo muhimu sana.

Usimamizi endelevu na ulinzi wa bahari na mazingira ya pwani na viumbe hai ni jambo muhimu ili kuiepusha jamii na athari mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi.
Source: Ismail Ngayonga
MAELEZO

Dar es Salaam.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO