SEKUNDE chache kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, pale Muhimbili, nilisikia sauti ndogo kama kengele ya fedha,nilitambua dakika ile kwamba baba yangu ameondoka.
Kabla ile sauti haijaondoka kabisa dakika ile nilishuhudia madaktari wakihangaika na muuguzi akikimbiza tenki la oksijeni nikajua kila kitu kimekwisha and now am alone.
Naam, leo kama tarehe ile Machi 10,2011 niliamka  asubuhi  hii  kumi na mbili na dakika 22, nikatoka kuona mahali ambapo baba yangu ana makazi yake ya kudumu, nikafadhaika, machozi yananitoka hapa ninapoandika it has never been the same any more.
Si rahisi kuelezea magumu yanayotokea katika maisha baada ya yeye kuondoka kwani yeye hakuwa tu baba alikuwa rafiki kwangu kwa watoto wake na wajukuu.
"Waambieni wajukuu zangu nawapenda sana" ilikuwa kauli yake akiwa hospitalini.
Alisema wakati nimeenda kumuona usiku mmoja pale hospitalini na rafiki yangu: kuwa na watoto kuzuri, akamshukuru Mungu wake, akasema wameweza kuleta marafiki zao kunifariji.
Katika hili sitaweza kumsahau Rehani Athumani, alikuwa kaka wa kweli kama makaka wengine akinitia moyo kwamba yatapita.
Lakini faraja ya watoto nikiwamo mimi, tuliobatizwa na kuamini Mafundisho ya Kanisa Katoliki na wajukuu na vitukuu inatokana na ukweli kuwa tuna  imani kwamba  yupo pamoja nasi akitusaidia kwa namna ya pekee, akitupelekea maombi yetu kwenye kiti cha enzi.
 Nasisi aliyetuacha hapa tunamuombea kwa Mungu kwamba yale aliyotaraji katika kumkiri Kristo ( 2 Wathesalonike 2:13-17) ndiyo anayofaidika nayo kwa sasa, akiwa naye paradise Amina.
Ama tukikumbuka mapenzi yake tunajiombea na sisi na nyie kwamba bwana wa amani atupe na amani kwa njia zote.
 Amina.Wasifu wa John Luwanda kwa Ufupi
John Luwanda alizaliwa katika miaka ya 1930 kijijini Nyandira, tarafa ya Mgeta mkoani Morogoro na kusoma shule ya msingi ya Nyandira mwaka 1950 hadi 1953.
Mwaka 1954 hadi 1957 alikuwa shule ya kati ya Bigwa mjini Morogoro ambako alimaliza darasa la nane. Mwaka 1958 aliingia shule ya sekondari ya Kwiro na kumaliza darasa la 10 mwaka 1959.
Mwaka 1960 alijiriwa kama Forest Ranger katika idara ya katika idara ya Misitu na kujiunga na Chuo cha Misitu cha Olmotony mwaka 1961.
Mwaka huo huo Julai aliacha kazi idara ya misitu na kujiunga na Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) kama fundi mitambo.
1968 alipandishwa cheo na kuwa studio assistant daraja la kwanza na mwaka 1970 Mei alipandishwa kuwa senior studio Assistant.
Mwaka 1971 alichukua mafunzo ya radio sound techniques yaliyoendeshwa kwa pamoja kati ya Radio Tanzania na na shirima la misaada la Sweden SIDA.
Februari 1974 alibadilisha kazi na kuwa mtangazaji.
Mafunzo ya utangazaji alichukulia kazini na baadaye kujifunza kuandaa utangazaji wa vipindi vya maigizo kutoka kwa mwalimu Mkanada ambaye alikuwa akifunza watangazaji na mwaka huo huo wa 1974 alipandishwa cheo na kuwa programme Officer daraja la pili. Mwaka 1977 alihudhuria mafunzo ya matangazo ya watu wa vijijini yaliyofanyika nchini Botswana na mwaka 1978 katika kujielimisha namna ya kuzuia ugonjwa wa kipindupindu, alitembelea Vietnam akiwa na wafanyakazi wa wizara ya afya.Desemba 1978 alipandishwa cheo na kuwa Programme Officer grade 1. Mwaka 1982 alipandishwa cheo kuwa senior programme officer grade 2.
Januari 1984 alihudhuria mafunzo nchini Malawi ya commercial advertsing production na hivyo kuongeza ujuzi wa utangazaji wa matangazo ya biashara. Septemba 1985 alipandishwa cheo na kuwa programme organiser na Desemba 1989 alihudhuria mafunzo Zimbabwe ya Commercial broadcasting.
Alistaafu kazi radio Tanzania miaka ya mwanzo ya 1990 na kuhamia Goba ambako aliishi akifanya shughuli za shamba hadi umauti ulipomfika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua kwa siku chache kisukari na kansa ya tezi ya kibofu.
Tutakukumbuka kwa upendo wako
Mungu aijaze roho yako na umande mbingu amina

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO