RAS Mtwara akifungua mafunzo
Katika kuongeza uwazi kwa jamii wito umetolewa kwa maafisa habari wa mikoa na halmashauri wa mikoa ya lindi,mtwara na Ruvuma kuanza  kutumia njia za haraka na za kisasa katika mawasiliano ikiwemo matumizi ya tovuti na mitandao ya kijamii ili kutangaza shughuli na mafanikio ya sera na mipango ya Serikali kwa wananchi.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza
Wito huo umetolewa leo na katibu tawala mkoa wa Mtwara,Bw Alfred Luandas wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa maafisa habari na wataalamu wa Tehama kwa mikoa hiyo katika mafunzo ya siku nane yatakayowezesha matumizi na uanzishaji wa tovuti ili kufikisha taarifa mbalimbali za serikali ikiwemo kutangaza shughuli za maendeleo na uwekezaji wa kiuchumi katika halmashauri za mikoa hiyo
Pamoja na kukabiliana na uwepo wa vyombo vingi vya habari ikiwemo mitandao ya jamii nchini na kuondoa urasimu wa utoaji wa taarifa kwa umma,Bw Luanda alieleza kuwa kuzinduliwa kwa tovuti hizo March 27 pia kutachangia kurahisisha mawasiliano kwa ukaribu na kwa gharama nafuu
Kwa upande wake kiongozi wa mafunzo hayo ambae pia ni Afisa Tehama Kutoka Tamisemi,Edgar Mdemu alieleza lengo la mafunzo hayo na umuhimu wa jamii kupata habari za serikali licha ya uwepo wa vyombo vya habari vya binafsi

Washiki wakiwa makini

‘Pamoja na mafunzo haya tunayowapa mategemeo yetu sasa utoaji wa taarifa za shughuli za umma zitawafikia wananchi kwa urahisi sana kutokana na uwepo wa teknolojia ya mawasilia kwa kuwa Dunia na mawasiliano kwa sasa yapo Kiganjani
Nao baadhi ya maafisa habari wa halmashauri mbalimbali katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma wamekiri kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa kwa ajili ya kazi zao za kihabari, hali ambayo inapunguza ufanisi katika kazi zao huku wakitoa wito kwa jamii kuanza kupata habari za halmashauri na mkoa kupitia tovuti zilizoanzishwa .
Mafunzo hayo ya  kuwajengea uwezo maafisa habari wa mikoa hiyo juu ya namna ya kuendesha tovuti za serikali kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3,chini ya ufadhili wa USAID Ili kumarisha sekta za umma Nchini

Source; Abdulaziz Video

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO