MFUKO ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF unadai malipikizo ya fedha zaidi ya  Sh tlirioni 2.5 kutoka kwa waajiri  zaidi ya 800 hapa nchini kufuatia kushindwa kwao kuwasilisha michango mara baada ya makato  kutoka kwa wafanyakazi wao kuanzia mwaka 2012 hadi kufikia Desemba 2016, imeelezwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji  NSSF , Bathow  Mmuni  alisema hayo  jana ( Machi 4) wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya  mgeni rasmi kufungua  semina ya siku moja kwa  Mahakimu, Mawakili wa Serikali na wa kujitegemea kutoka mikoa ya   Dar es Salaam na Morogoro iliyoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika katika  Jengo la NSSF mkoa wa Morogoro.

Mgeni  rasmi katika ufunguzi huo alikuwa ni mkuu wa mkoa huo, Dk Kebwe Stephen Kebwe ambaye aliwakilishwa Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa anayeshughulikia  Uchumi  na Uwezeshaji , Ernest Mkongo na ilihusu utoaji wa elimu,  uelewa mpana wa  majukumu ya NSSF kwa wanachama na  taifa ambao ni mpango endelevu  wa utiaji wa elimu hiyo kwa makundi mbalimbali likiwemo la  Mahakimu, Mawakili wa Serikali na wa kujitengemea.

Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji  NSSF alisema ,pamoja na mpango wa kutoa elimu  kwa wanachama , waajiri na makundi mengine kuhusu majukumu ya NSSF , bado changamoto kubwa ni kwa waajiri  wengi kushindwa kuwasilisha michango ya makato ya fedha katika mfuko huo.

Alisema kitendo hicho kimakuwa kilileta adha na  usubufu kwa wafanyakazi pale wanapostaafu kwa kuwa wanashindwa kulipwa mafao yao kwa wakati kwa kuwa mwajiri hakuwasilisha michango  na matokeo yake lamawa zote zinaelekwa NSSF. 


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO