Katika kuelekea siku ya uzinduzi huo ambao kwa kanda ya kusini utakaofanyika mkoani Mtwara Machi 27 mwaka huu, wizara ya nchi ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma Nchini PS3, imeendesha mafunzo kwa maafisa habari wa ofisi za wakuu wa mikoa pamoja na halmashauri juu ya matumizi ya tovuti, ambapo miongoni mwawashiriki wameeleza  kunufaika na mpango huo utakaojenga utawala bora.
Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya washiriki wameshukuru Mradi wa PS 3 Kwa kuwezesha sekta za umma kuwa na tovuti ambazo zitaanza kuwa hai ifikapo March 27 na kusaidia maafisa habari kuanza kuwajibika ili jamii iweze habarika na fursa mbali mbali bila gharama kubwa.


Aidha walieleza kuwa Wakati serikali ikielekea katika uzinduzi wa matumizi ya Tovuti katika ofisi za umma ikiwa ni pamoja na ofisi za mikoa na halmashauri, Tayari baadhi ya wananchi mkoani Mtwara wamepongeza hatua hiyo na kudai kuwa itasaidia kuwapo kwa uwazi katika upatikanaji wa taarifa.
wananchi hao wamesema kutokana na kuwapo kwa utandawazi unaochangiwa na kupanuka kwa teknolojia ya mawasiliano, wananchi watanufaika na huduma hizo za Tovuti katika kupata taarifa ambazo hazina ulazima wa kuzifuatilia katika makao makuu ya ofisi husika.
Mafunzo hayo ambayo yameanza Machi 20 kwa kuhusisha maafisa habari na maafisa TEHAMA kutoka katika mikoa ya Mtwara, lindi na Ruvuma yanatarajiwa kuhitimishwa Machi 27 mwaka huu ikifuatiwa na zoezi la uzinduzi wa tovuti hizo.
Source: Na Abdulaziz video,MtwaraPost a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO