SHIRIKISHO la Soka la Argentina (AFA) limeahirisha mechi za ligi kuu kutokana na wachezaji kuingia katika mgomo baada ya majadiliano ya kushawishi kusiwepo na mgomo kuvunjika.

Imeelezwa kuwa vilabu vingi nchini humo vimekumbwa na tatizo kubwa la kifedha na hivyo kushindwa kulipa mishahara ya wachezaji kwa miezi kadhaa sasa. 

Umoja wa wasakata kabumbu  nchini humo umesema kwamba wachazaji wataendelea na mgomo hadi hapo kitakapoeleweka.

Mgomo huo unaendeshwa na wachezaji wa vilabu takribani 200 nchini humo.

Mechi ngumu zilizoahitishwa ni za Rosario Central v Godoy Cruz, zilizokuwa zifantyike katika mji wa Rosario, na San Lorenzo v Belgrano, zilizokuwa zifanyike mjini Buenos Aires. Mechi zote hizo zilikuwa zifanyike Ijumaa.

Mgogoro huo umeelezwa kuwa ulianza baada ya Ofisa mwandamizi wa AFA kutajwa katika sakata la rushwa katika haki ya kutangaza soka kwa njia ya televisheni.

Msimu wa ligi ulikuwa uanze miezi kadhaa iliyopita baada ya kuisha kwa majira ya kiangazi lakini mgogoro huo ulichelewesha kuanzwa kwa msimu mpya wa ligi  hadi Ijumaa na kulazimika kuahirisha tena kutokana na mgomo huo.

Ili kumaliza mgogoro serikali ya Argentina inayoongozwa na  Mauricio Macri , Alhamisi walilipa dola za Marekani milioni 22 kwa AFA ili wachezaji wawezwe kulipwa lakini chama cha wachezaji kilisema fedha hizo hazitoshi.

Walisema kwamba viongozi wa klabu hizo walikopa fedha nyingi kuliko walivyotakiwa na hivyo hawakubali.

Mgogoro wa soka wa Argentina umeanza baada ya kifo cha Julio Grondona mwaka 2014 ambaye aliongoza AFA kwa miaka 35.

Kiongozi huyo ambaye pia alikuwa Makamu wa rais wa FIFA yumo pia katika kundi la uchunguzi unaofanywa na Marekani dhidi ya FIFA kwenye tuhuma za rushwa.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wamesema kwamba wakati wa uhai wake Grondona  alikuwa ni mtu anayehakikisha kwamba soka la Argentina haliyumbi.

Hata hivyo wengi wanaamini kwamba mgomo wa wachezaji ni tatizo lakini ni kitu muhimu katika kuhakikisha kwamba haki inatendeka katika soka.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO