Wanafunzi 2,348 waliokata rufaa katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu  wameshinda rufaa zao .

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji  wa bodi ya mikopo, Abdul-Razaq Badru rufani zuilizoshinda ni miongoni mwa rufaa 20,020 zilizopokelewa na  kwa njia ya mtandao.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa jana  imesema kuwa katika kipindi cha kati ya Novemba 1, 2016 na  Januari 31, 2017 jumla ya rufaa 20,020 ziliwasilishwa kwa njia ya mtandao.

Imeelezwa kuwa kati ya hizo, jumla ya fomu za rufaa 17,020 zilipokelewa kutoka vyuoni zikiwa na viambatisho muhimu.

Aidha ilisemwa kuwa Mapitio ya rufaa zilizowasilishwa yalifanywa kwa fomu zote zilizopokelewa.

Mkurugenzi huyo alitaja matokeo ya rufaa hizo (zilizoshinda) kwa makundi kuwa ni: Walemavu 61; Yatima 57; Wenye mzazi mmoja 570; Familia zenye kipato duni 1,169 na Waliosomeshwa na wahisani 491. 


Kwa mujibu wa taarifa hiyo Bodi ya Mikopo tayari imetuma vyuoni majina ya wanafunzi walioshinda rufaa zao na inaendelea kukamilisha malipo ya mikopo yao.

Aidha, Bodi imesema kwamba zoezi hilo kwa sasa limefungwa rasmi hadi hapo litakapotangazwa tena katika mwaka ujao wa masomo.

Taratibu za upangaji na utoaji mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu,zinatoa fursa kwa waombaji ambao ama hawakupata mikopo au wamepata kiwango cha mikopo wanachoona hakikidhi mahitaji, kukata rufaa.

Kwa mujibu wa taratibu zilizopo, waombaji hupewa siku tisini (90) kuanzia mwanzo wa mwaka wa masomo kuwasilisha rufaa zao.  Rufaa hizo huwasilishwa kwa njia ya mtandao na vielelezo/viambatisho huwasilishwa kupitia madawati maalum ya mikopo vyuoni. 

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO