TAASISI ya Kimataifa ya Kilimo cha Kitropiki (IITA) imefanikiwa kupata aina nne ya mbegu za muhogo ambazo haziathiriwi na magonjwa makubwa ya zao la muhogo ukiwamo michirizi ya kahawia .

Mbegu hizo ambazo zimeonekana kufaa kwa sasa zinasubiri utaratibu wa serikali ili ziweze kuwafikia wakulima wengi zaidi.

Wakulima wamekuwa wakipoteza mamilioni ya shilingi kutokana na ugonjwa huo ambao umekuwa ukisumbua nchi na wataalamu wanasema ugonjwa huo unasababisha hasara ya  dola za marekani milioni 50 kwa mwaka sawa na shilingi bilioni 110.

Kwa mujibu wa maelezo ya wataalamu katika maabara ya kisasa ya kimataifa ya IITA mjini hapa, ugonjwa huo ambao unasababishwa na virusi ulikuwapo toka mwaka 1931, lakini ukaibuka na kuwa tishio katika kipindi cha miaka 10 iliyopita .

Kwa miaka miwili sasa IITA imelekeza nguvu zake kutafuta dawa za ugonjwa huo na kuja na suluhu ya mbegu ambayo ni safi na pia kutumia wadudu wengine kukabiliana na wadudu waharibifu wanaosababisha magonjwa ya muhogo.

Mtaalamu wa IITA anaye shughulikia virusi vya mimea, Dk James Legg  akizungumza amesema kwamba juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo zimefanyika katika maabara hiyo ya dar es salaam na kuja na namna mbili za kuudhibiti za kuwa na mimea ambayo haithiriki na ugonjwa na pia kutumia njia za kibaiolojia ambapo wadudu wanazalishwa na kupelekwa mapema katika mashamba kukabiliana na wadudu waharibifu.Dk Legg akizungumza na waandishi wa habari walioalikwa katika maabara hiyo kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali za kusaidia wakulima kukabiliana na matishio mapya ya magonjwa na mabadiliko ya hali ya hewa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya uwapo wa IITA alisema muhogo unakabiliwa na tishio kubwa kama wakulima wasipoelekezwa namna ya kukabiliana na magonjwa.

Alisema kwamba maabara yao ambayo ilifunguliwa na Rais Jakaya Kikwete kwa sasa ina vifaa bora zaidi za kufanyia utafiti na baadhi ya mashine zinapatikana katika maabara ya Afrika Kusini kwa nchi zilizokusini mwa Jangwa la sahara.

“Tunaamini tutafanikiwa kudhibiti magonjwa makubwa ya muhogo yanayotia hasara wakulima kwa kuwa tumeweza kupata mbegu zinazostahili kupandwa, mbegu ambazo hazina magonjwa...Tunashauri wakulima wasitumie mbegu zao kwa kuwa hawawezi kutambua kwamba zimeathirika,” anasema Dk Legg.

zao la muhogo ni muhimu nchini Tanzania likiwa la pili kutoka mahindi kwa uzalishaji.Aidha zaidi ya asilimia 80 ya wakulima wadogo wanaotegemewa nchini kwa kulisha wanapanda mihogo wakizalisha takribani tani milioni 4.5 za muhogo kila mwaka.

Karibu robo tatu ya muhogo inazalishwa kwa ajili ya chakula, kiasi kinatumika kulisha mifugo na matumizi ya viwandani. Mara nyingi muhogo hutumiwa kama akiba ya chakula wakati wa ukame au baa la njaa.

Pamoja na umuhimu wake huo wakulima wa Tanzania hupoteza tani milioni 2.5 za muhogo kutokana na ugonjwa wa mchirizi ya kahawia (CBSD), Batobatokali cassava mosaic disease (CMD) na  cassava green mite (CGM).

Mtaalamu wa uzalishaji wa muhogo wa IITA, Dk Edward Kanju, anasema kwamba kutoka katika aina 30 z ambegu ambazo zimefanyiwa mkajaribio , aina nne zinaonekana kufanya vyema katika majaribio kwenye mashamba na anadhani zikiopelekwa kwa wakulima zitaweza kabisa kukabiliana na magonjwa hasa katika uklanda wa ziwa ambako hali si barabara.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO