KUNDI kubwa la watu waliokuwa katika sherehe za harusi walipona shambulio la bomu la kujitoa mhanga baada ya mbwa  aliyekuwa katika eneo hilo kula sahani moja na mdada ambaye alikuwa amebeba mabomu.

Mdada huyo inaaminika ni mmoja wa wapiganaji wa Boko Haram.

Tukio hilo la mjini Maiduguri ambalo limeripotiwa na Naija.News linasema mbwa huyo alikuwa ni wa nyumba ya jirani.

Mdada huyo ni miongoni mwa wahanga watatu waliokuwa wakijaribu kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ambao walijilipua wenyewe baada ya mambo kwenda kinyume.

Matukio hayo yalifanyika jana Jumapili  ya Aprili 2 .

Kwa mujibu wa Polisi, tineja huyo aklikuwa anajipeleka katika hafla hiyo wakati mbwa alipomvamia na kuanza kukukurusana naye na hivyio kujilipua yeye na mbwa huyo.

Imeelezwa kuwa msichana huyo alifyatua mkanda wa mabomu aliouvaa wakati akikabiliana na mbwa huyo ambaye alikuwa tayari amemdhibiti asifike kwenye kundi la watu.

Pia imeelezwa kuwa tukio la saa moja na nusu asubuhi lilifanyika katika jamii ya Belbelo huko Jere katika jimbo la Borno.

Msemaji wa Polisi katika jimbo la Borno, Victor Isuku alithibitisha habari za tukio hilo ingaa hawakusema kama mbwa huyo alikuwa amepewa mafunzo maalumu.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO