SAKATA la kampuni ya kufua umeme ya Richmond lililosababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, limeibuka upya bungeni huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa ya Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akisema, `Lowassa hasafishiki’.

Aidha, Dk Mwakyembe amesema yeyote mwenye hoja za msingi za kutaka kumsafisha Lowassa afufue sakata hilo kwa kuzileta bunge na kwamba yuko tayari kumwomba Rais John Magufuli amweke pembeni katika baraza la mawaziri kwa muda ili apate muda wa kushughulikia suala hilo ambalo anasisitiza kamati yake ilifuata taratibu zote za msingi katika kukusanya ushahidi.

Wakati wa sakata hilo, Dk Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela,
ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Bunge iliyoshughulikia sakata la Richmond.

Dk Mwakyembe aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana wakati akijibu
hoja iliyotolewa juzi na Nassari akimtuhumu kutotenda haki wakati
akishughulikia sakata la Richmond.

Alisema kilichowasilishwa na kamati yake wakati huo mbele ya Bunge
kilizingatia utaratibu wa kisheria na kwamba hakina upungufu wala
haikulenga kumwonea yoyote kama inavyodaiwa.

 “Mheshimiwa yamesemwa mengi hapa, lakini ni vyema tukaweka sawa ili
tusiupotoshe umma.
  Kuna suala la suala la Richmond. Hili suala
limeibuliwa na Nassari (Joshua, Mbunge wa Arumeru Mashariki- Chadema) anailalamikia Kamati kwamba haikumtendea haki Lowassa katika sakata la Richmond. Nasema ni kazi ngumu kutaka kumsafisha Lowassa…kwa kuwa alitambua hili, pengine ndiyo maana ilibidi anywe Konyagi.

“Analalamika Lowassa angehojiwa, angehojiwa vipi wakati
tulishajiridhisha? Hili lilishakwisha. Kazi ya Kamati ilikuwa
kuchunguza, siyo kuchukua uamuzi. Sasa aliyetakiwa kuhojiwa
alijiuzulu, mnataka kumlaumu Mwakyembe kwa hilo? Hatukuona sababu ya kumhoji Lowassa, tulikuwa na ushahidi.

“Nasema hivi, kama akipatikana jasiri wa kufufua hili jambo ili mambo
yawe hadharani, akiwa na ushahidi alete hilo suala hapa bungeni kama
atutawanyoa kwa chupa. Madoa ya lami hayaondolewi kwa kutumia katani,”
 alisema.

 “Kama yupo mwenye hoja za msingi anayekereketwa na suala la Richmond aziwasilishe hapa kwa kuzingatia utaratibu ili zifanyiwe kazi.

“Ikitokea hivyo, nitamwomba Rais aniweke pembeni uwaziri ili
nilishughulikie suala hili hadi nitakapolimaliza. Nalisubiri kwa
hamu,”
 alisema Dk Mwakyembe na kuongeza kuwa, walijiridhisha kwa
kukusanya nyaraka 104, lakini pia walihojiwa watu 75 walioulizwa
maswali zaidi ya 2,717.

Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu Februari 7, mwaka 2008 kutokana na
kashfa ya Richmond, akitajwa kuhusika kuibeba kampuni hiyo ili ipate
zabuni ya kufua umeme na kuuza kwa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco).

Awali, Mbunge Job Lusinde (Mtera-CCM) alipokuwa akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Tamisemi na Utawala Bora, aliitaka kambi ya upinzani kumchukulia hatua Nassari (bila ya kumtaja jina) kutokana na kitendo hicho.

Lusinde aliitaka kambi hiyo kufuata nyayo za serikali ilipoamua
kumwondoa kwenye uwaziri aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kwa tuhuma za kuingia bungeni akiwa amelewa.

“Nanyi sasa fuateni nyayo za CCM na serikali kwa kumchukulia hatua
mbunge wenu kama ambavyo ilifanyika kwa Kitwanga ambaye hakukutwa na chupa, lakini alichukuliwa hatua,”
 alisema.
https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/images/cleardot.gif


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO