WAJASIRIMALI wadogo 200 wa Manispaa ya Songea wamepata mafunzo ya siku mbili ya usalama na afya mahali pa kazi  ambayo yametolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi(OSHA).
Mkurugenzi wa Mafunzo,Utafiti na Takwimu wa OSHA Joshua Matiko akizungumza kwenye mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Songea Club,alisema OSHA imekuwa na desturi ya kutumia mwezi Aprili kila mwaka kuelezea kazi mbalimbali zinazolenga kuboresha hali ya usalama na afya mahali pa kazi.
Alisema kila mwaka Aprili 28 ni siku ya maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahali pa kazi duniani ambapo OSHA hutumia maadhimisho hayo kuhamasisha usajiri wa maeneo ya kazi,vikao vya wadau na makongamano ya watalaam wa masuala ya afya na usalama.
“Tunatumia maadhimisho hayo pia kwa kutoa vipindi vya elimu katika vyombo vya habari,maonesho ya usalama na afya na mafunzo ya usalama na afya kwa wajasirimali wadogo kama inavyofanyika hapa Songea’’,alisema Matiko.
Hata hivyo alisema mafunzo hayo ambayo yanatolewa bure yamelenga kuziba mwanya wa elimu ya usalama na afya kazini uliopo baina ya Taasisi na kampuni katika sekta rasmi na wazalishaji wadogo ambao hawajaweza kufikiwa katika mfumo rasmi wa serikali wa kusimamia afya na usalama wa wafanyakazi.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo,mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dk.Binilith Mahenge amewapongeza wakala wa serikali OSHA kwa kuanzisha mpango wa mafunzo hayo ambapo amewaomba waangalie uwezekano wa kuyaboresha zaidi mafunzo hayo ili yawafikie watanzania wengi.
Kwa upande wake Meneja wa OSHA Kanda ya Kusini Wilbert Ngowi alisema Mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo ya afya na usalama mahali pa kazi ambayo yalifanyika mwaka jana katika nchi nzima  yakishirikisha jumla ya wajasiriamali wadogo 1830 ambapo mwaka huu mafunzo hayo yameshirikisha wajasirimali wadogo 2500.
Kulingana na Ngowi,wajasirimali hao wamejifunza mada mbalimbali zikiwemo majukumu ya msingi yanayofanywa na OSHA,maana ya usalama na afya mahali pa kazi,namna ya kuvitambua vihatarishi vilivyopo sehemu za kazi,kujikinga na ajali na elimu ya huduma ya kwanza.
Source: Albano MideloPost a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO